Friday 18 June 2010

MISOSI MISOSI LUNCH TIME HII LEO

Mchuzi Wa Nazi Wa Nguru Na Bamia Samaki nguru 5 vipande



Thomu na Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagawa kijiko cha supu
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha chai
Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha chai
Ndimu 2 kamua maji
Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Nguru

1. Changanya vitu vyote katika kibakuli ufanye masala ya kupaka kwenye samaki.
2. Roweka kwa muda nusu saa
3. Paka treya mafuta, kisha mpange nguru na mchome katika oveni.
4. Atakapoiva upande upande mmoja mgeuze upande wa pili huku unanyunyizia mafuta.
5. Epua weka kando.

Vipimo Vya Mchuzi Wa Nazi
Vitunguu maji 2
Nyanya 2
Tuwi zito la nazi 2 vikombe viwili

Bamia 1 kikombe
Haldi (bizari ya manjano) ¼ kijiko cha chai
Pilipili mbichi 1
Ndimu kiasi
Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mchuzi



1. Katika sufuria tia tuwi kikombe kimoja, kisha tia bamia ulizokatakata zipike ziwive kidogo.
2. Saga kitunguu, nyanya na pilipili mbichi katika mashine ya kusagia (blender) kisha mimina katika tui la bamia.
3. Tia vipande vya nguru, bizari, chumvi, ndimu, kisha tia tui lilobakia.
4. Acha mchuzi uchemke kidogo kidogo kisha epua utie katika bakuli ukiwa tayari.

No comments:

Post a Comment