Thursday 17 June 2010

MNAWAKUMBUKA HAWA WATAALAM WA MUZIKI?

mtaaluma loketo nae alikua mbaya enzi zake,akiingia na kitana basi na zile style zake anazuga kama anaanguka halafu anatoa kitana anachana nywele si mchezo,mambo ya tulemonde loketo e e loketooo,tulemonde washiwaa e e washiwa ilikuwa raha mpaka kisogoni dah.
yondo sister enzi hizo mbuta mutu mwana mama eeh mamaaanalingakayo mwana mama eeh mama,likitandikwa solo hapo utakimbia,kipindi hiyo nakaa temeke tazara jirani na njaro uswazi kulikua na baa ya tap tap basi ni mbuta mutu mpaka kichwa kinauma.

kanda bongo man,jamaa kwa sasa anajipigia boksi lake manchester UK,magitaa kayatupilia mbali.

No comments:

Post a Comment