Wednesday, 20 February 2013
KATIBU MKUU WA BARAZA LA MITIHANI ADAI CLOUDS FM IMECHANGIA UANDIKAJI WA MATUSI KWENYE MTIHANI YA FORM 4 MWAKA HUU...!!!
Katibu mkuu wa baraza la mitihani la taifa, Bi Joyce Ndalichako, amekilaumu kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa kilimpa promotion kijana aliendika matusi na "Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.
Katibu mkuu huyo amedai kuwa hatua hiyo ya Clouds FM imechangia uandikaji wa matusi kwa watahaniwa wa mwaka huu.
Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.
Source: Clouds FM asubuhi ya leo.
MTUHUMIWA WA MAUAJI ANAPOJIPELEKA POLISI NA KUAMBIWA TUMEFUNGA NJOO KESHO!
wahenga walisema ukistaajabu ya firauni utayaona ya musa,hiyo ilidhihirika hapa sweden maana kuna visa ambavyo ni made in hapa hapa vinachekesha kama sio kusikitisha.
wiki hii kumekuwa na matukio kadhaa ya kushangaza
1.ni pale vibaka walipoenda kuvamia duka la saa kwa nia ya kuiba huku wakiwa hawana silaha yoyote zaidi ya kujivisha sox usoni.ndio maana hapa ni kujaribujaribu tu,wameona wenzao wanaweka bag nje na kuandika bomb na wanaondoka na mali kibao huku polis wakiogopa kusogea kwanini na wao wasijaribu.mara hii vijana hao waliishia mikononi mwa polis baada ya kukamatwa kama kuku wanaoumwa mdondo.hongera hapo kwa polis wa sweden.
2ni pale ilipokuja gundulika kwamba kumbe yule gaidi aliyetaka kulipua mamia ya watu hapo central station mwaka 2010 alikuwa siku zote za maisha yake anaishi kwa kufadhiliwa na pesa za serikali yasweden za msaada wa wanafunzi.mpaka siku anajilipua huyu bwana alikua na deni la zaidi ya koronar 750,000/=.na inasemekana siku mbili tu kabla ya kujilipua na jaribio lake kuua watu kushindwa.walikua wamemtumia tena 57,000/= koronar.thanx kwa serekali ya kiswede.
3.kubwa kuliko ni hii ambapo jamaa mmoja huko goteborg amekuwa wanted baada ya kumpiga risasi mmoja wa viongozi wa vikundi vya mafia huko.huyo bwana baada ya kuishi kwa kujificha ficha kwa muda mrefu akaamua ajipeleke polisi mwenyewe akashtakiwe.kufika polisi polisi wakamjibu kwamba "e bwana sisi tumefunga bana tunafanya marekebisho njoo kesho".jamaaa akajiondokea zake,baada ya siku 2-3 huyu bwana alipokutana na waandishi wa habari na kukutwa akizurula mitaani alipoulizwa akasema "mabwege wale,nimejipeleka wanasema wamefunga kituo mpaka kesho.mwandishi alipomwambia sasa si wamefungua uende akajibu"nani aende!?mi mwenyewe nshaghairi kufungwa"
haya habari ndio hizo nawahi box
Tuesday, 19 February 2013
KANISA LINGINE LACHOMWA MOTO ZANZIBAR

WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, amesema leo kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku. Amesema moto huo ulizuka mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa likishambuliwa kwa mawe juu ya makapaa.
Amesema baada ya mlinzi huyo kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea. Kamanda Olomi amesema kuwa wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea, mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.
Amesema Polisi walipofika hapo walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa kanisani hapo. Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.
Hata hivyo amesema uimara wa dali lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa na kuliteketeza kabisa kanisa hilo. Amesema wakati uongozi wa kanisa hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Olomi amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matishio mengine kama hayo.
MAMBO YA SKYLIGHT BAND NDANI YA THAI VILLAGE

Pichani juu na chini ni Sony Masamba, Mary Lukas, na Joniko Flower wakitumbuiza mashabiki wa Skylight Band kwenye kiota cha Thai Village kinachowakusanya mashabiki kila Ijumaa ya wiki kutoka sehemu mbalimbali za jijini la Dar na vitongoji vyake.
Burudani ikiendelea.
Sony Masamba ndani ya hisia kali kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ile kitu roho inapenda.
Umeshawahi kusikia kipaji cha huyu dada…??? ni Aneth Kushaba AK 47 akiwajibika kazini, njoo Ijumaa moja ujionee mwenye.
Eric Ndalu akishow love na mdau.
Tumia pesa ikuzoeee. Vijana wanaojua kula bata mjini hawakosekani Kila Ijumaa wako na Skylight Band.
King Kif meno 32 yote nje anapoona wadada wazuri kama hawa.
Pichani juu na chini mashabiki wa Bendi inayoshika kasi mujini Skylight wakijimwaga na masebene yaliyokuwa yakiporomoshwa na Sony Masamba pamoja na Joniko Flower.
Joniko Flower akitoa buradani huku akisindikizwa na Aneth Kushaba AK47 pamoja na Mary Lukas.
Haki Ngowi (katikati) akishow some love na Fans wa Skylight Band Julio (kushoto) na Gideon (kulia).
Hayo yote ni mapenzi na Skylight Band….. Mdau akiwa ametweta jasho baada ya kusakata Sebene vilivyo akiona ashow love na dada zake.
Couples waliobamba kwenye Show ya Skylight Band wakishow love mbele ya Camera yetu…Karibuni tena.
Salma Yusuf akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band na mambo ya pwani (mduara) huku akipewa Sapoti na Mary Lukas sambamba na Sam Machozi.
Kijana David akianza kuonyesha woga wa kuzungushiwa nyonga huku akiwa amekaa.
Hapo sasa Kijana David akiwa ameelemewa: Warembo wa jijini Dar wakimpagawisha kijana na kumtoa jasho la pua.
Mwanadada akiwatoa jasho wanaume wawili wakati wa mduara shurti kuzungusha nyonga, haswa ukiwa nayo na dada yetu hapo amejaaliwa ndio raha ya kupitia unyago hiyo.
Hapo sasa twende kazi……..
Aneth Kushaba AK47 akishow love na Ceaser wa Clouds Tv pamoja na Dj Choka ambao ilikuwa mara yao ya kwanza kushuhudia Live Performance ya Skylight Band kwenye kiota cha Thai Village.
Bongo Flava nao ni moja wa mashabiki wa Skylight Band….Hemedy a.k.a PHD na Gelly wa Ryhmes walikuwepo kushow love na Skylight Band.
Dada Wendo all the way from Ughaibuni akishow love na mdau.
Joniko Flowe wa Skylight Band na fans wake.
Joniko Flower, Hemedy pamoja na Gelly wa Rhymes wakishow some love.Chanzo:
moeblog
Subscribe to:
Posts (Atom)























