Wednesday, 20 February 2013

MTUHUMIWA WA MAUAJI ANAPOJIPELEKA POLISI NA KUAMBIWA TUMEFUNGA NJOO KESHO!

wahenga walisema ukistaajabu ya firauni utayaona ya musa,hiyo ilidhihirika hapa sweden maana kuna visa ambavyo ni made in hapa hapa vinachekesha kama sio kusikitisha.

wiki hii kumekuwa na matukio kadhaa ya kushangaza

1.ni pale vibaka walipoenda kuvamia duka la saa kwa nia ya kuiba huku wakiwa hawana silaha yoyote zaidi ya kujivisha sox usoni.ndio maana hapa ni kujaribujaribu tu,wameona wenzao wanaweka bag nje na kuandika bomb na wanaondoka na mali kibao huku polis wakiogopa kusogea kwanini na wao wasijaribu.mara hii vijana hao waliishia mikononi mwa polis baada ya kukamatwa kama kuku wanaoumwa mdondo.hongera hapo kwa polis wa sweden.

2ni pale ilipokuja gundulika kwamba kumbe yule gaidi aliyetaka kulipua mamia ya watu hapo central station mwaka 2010 alikuwa siku zote za maisha yake anaishi kwa kufadhiliwa na pesa za serikali yasweden za msaada wa wanafunzi.mpaka siku anajilipua huyu bwana alikua na deni la zaidi ya koronar 750,000/=.na inasemekana siku mbili tu kabla ya kujilipua na jaribio lake kuua watu kushindwa.walikua wamemtumia tena 57,000/= koronar.thanx kwa serekali ya kiswede.

3.kubwa kuliko ni hii ambapo jamaa mmoja huko goteborg amekuwa wanted baada ya kumpiga risasi mmoja wa viongozi wa vikundi vya mafia huko.huyo bwana baada ya kuishi kwa kujificha ficha kwa muda mrefu akaamua ajipeleke polisi mwenyewe akashtakiwe.kufika polisi polisi wakamjibu kwamba "e bwana sisi tumefunga bana tunafanya marekebisho njoo kesho".jamaaa akajiondokea zake,baada ya siku 2-3 huyu bwana alipokutana na waandishi wa habari na kukutwa akizurula mitaani alipoulizwa akasema "mabwege wale,nimejipeleka wanasema wamefunga kituo mpaka kesho.mwandishi alipomwambia sasa si wamefungua uende akajibu"nani aende!?mi mwenyewe nshaghairi kufungwa"

haya habari ndio hizo nawahi box

No comments:

Post a Comment