Friday, 8 February 2013

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU NAZARETH MWAMGOGWA

               MAREHEMU NAZARETH MWAMGOGWANI MIAKA 25 SASA IMEPITA TANGU ULIPOTUTOKA RASMI HAPO TAR 06-02-1988.SISI WANAO ISAAC,SUMA,IMMA NA REBECCA TUNAKUKUMBUKA DAIMA.KWA MAJONZI TULIYOKUWA NAYO ULIPOTUACHA GHAFLA KWA AJALI HATUKUDHANI KAMA ITAFIKA SIKU KAMA YA LEO IKIWA NI MIAKA 25 IMEPITA TUKIWA WOTE BADO HAI.KWA UWEZA WA MWENYEZI MUNGU WOTE BADO TUKO HAI NA AFYA NJEMA.NAFASI YAKO MIOYONI MWETU ITAENDELEA KUWEPO MPAKA HAPO TUTAKAPOKUTANA TENA.UTAENDELEA KUKUMBUKWA KWA UCHESHI WAKO NA UNADHIFU WAKO BILA KUSAHAU NGUVU ZAKO KATIKA KUSIMAMIA HOJA UNAYOIAMINI.
WANAO BADO TUNAENDELEA NA TUTAENDELEA KUSIMAMIA UKWELI NA KUSAHIHISHA PALE TUNAPOONA HAPAENDI SAWA.
UNAKUMBUKWA NA NDUGU WOTE SIKU ZOTE HASA MAMA YAKO TUKUSUMA MWAKINGWE,WADOGO ZAKO ELLY NA RUBEN,BILA KUSAHAU WANAO WENGINE BARAKA NA TULLY.
TUNAENDELEA KUKUOMBEA KWA MUNGU AKUPE MAISHA MEMA NA YA AMANI HUKO ULIKO MPAKA HAPO TUTAPOONANA TENA

MUNGU AILAZE ROHO YAKO PEMA.AMEN

R.I.P.BABA 

2 comments:

 1. Pole sana kaka Isaac na familia yote..MUNGU ataendelea kuwatunza na kuwabariki.

  Ulale kwa Amani baba NAZARETH MWAMGONGWA.

  Nafikiri uliachwa mdogo sana kaka Isaac.

  ReplyDelete
  Replies
  1. asante sister,yah nilikua bado mdogo sana.ndo maisha tena

   Delete