Thursday 7 February 2013

MELI YA MV VICTORIA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO



MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.

Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.

Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.

Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.

Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.

Hii ndiyo sehemu iliyokuwa na mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea ndipo cheche za moto zikapenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuzua motomkubwa.

Juhudi zikiendelea kwa maafisa wa kikosi hicho kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.

Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.

Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.

Hata hivyo moto huo uliodumu kwa saa kadhaa ulifanikiwa kuzimwa ndipo juhudi za kuyatoa magodoro na mito yote ya makochi yaliyokuwemo ndani ya hifadhi ya mizigo ili kuhakiki uharibifu pamoja na kufanya tathimini kwa mali zilizo haribika.
Kwa umakini zaidi kuhakiki moto huo.
Wafanyakazi wa MSC wakitumia mashine maalumu ya kushushia mizigo ya kampuni hiyo wakitoa mabaki ya vitu vilivyounguzwa na moto.
Mtoto huo kama ungefanikiwa kuiteketeza meli ya Mv Victoria ingekuwa hasara kubwa sana kwa shirika la Marine Service kukosa chombo cha usafiri majini bandari za miji ya Mwanza, Kemondo na Bukoba, kwani  meli hii ndiyo meli pekee iliyosalia kwa safari hizo.

Ikumnbukwe kuwa Mv. Serengeti kwa sasa haiko shughulini na Mv. Bukoba ndiyo hivyo tena ilizama mwaka 1996 na mamia ya ndugu zetu.

Juhudi za ushushaji mizigo iliyoungua zikiendelea.



Ndani ya masaa mawili moto huo ulikuwa umedhibitiwa na kikosi cha zima moto na uokoaji waliowasili katika eneo hilo muda mchache baada ya moto kuanza wakitumia gari lenye namba za ausajili STK 1965 Mali ya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Mmliki wa magodoro pamoja na mito ya makocho iliyoteketea kwa moto aliyejitambulisha kwa jina moja la Ogunya amesema kuwa amepoteza magodoro 180 pamoja na mito 80 katika tukio hilo.


Kwa upande wake afisa mfawidhi wa Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa majini na nchi kavu(SUMATRA) kanda ya ziwa Josephat Loisimaye amesema kuwa uzembe wa viongozi wa MSC ndio ambao ulisababisha kutokea kwa moto huo.

Amesema kuwa viongozi wa MSC walipashwa kuchukua tahadhari mapema kabla ya kuanza uchomeleaji katika sehemu ya Meli hiyo na kueleza kuwa wanasubiri ripori ili waweze kuchukua hatua zaidi.

Hata hivyo Loismaye amesema kuwa Meli ya Mv Victoia iko salama na itaendelea na safari zake kwenda Bukoba leo usiku kwa kuwa moto huo haukuweza kuathiri mfumo wa injini ya Meli na kukipongeza kikosi cha zimamoto kutokana na kufika mapema na kuzima moto huo vinginevyo Meli hiyo ingeliteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa

michuzi-matukio

No comments:

Post a Comment