Tuesday, 12 February 2013

TUKIO LA MAJAMBAZI KUPORA JANA BREDANG KATIKA PICHA
tukio la majambazi kupora jana hapo bredang stockholm limeshtua wengi maana sasa imekua kawaida kwa matukio kama hayo kutokea hapa.zamani haikuwa hivi ila kwa sasa inatokea mara kwa mara.tukikumbuka mwezi uliopita tu kuna wengine walikamatwa na mmojawao kuuliwa kule sodertaje.pia kuna matukio mengine mawili yanafanana na hili yametokea fittja na masmo.
walichofanya jamaa wamekuja na bag la mjapan wameliandika "BOMB"wakaliacha njiani.(askari wa kiswede hapo hawasogei)
kisha wakavunja milango na caterpillar walilokuja nalo wakazama nalo mpaka ndani wakazoa dhahabu kiasi cha kutosha kisha wakatokomea zao na volvo.hawakufika mbali wakaliacha lile volvo na wakaondoka kwa njia nyingine wanayojua wao.polisi walitaarifiwa mapema tu na raia wema lakini walipofika wakaanza kusua sua mpaka jamaa wamekimbia.
tukio hili limesababisha usumbufu mkubwa kwani tren red line ilifungwa kwa muda wa masaa kadhaa.mi nikiwa mmojawapo wa wahanga.
juhudi za kuwatafuta majambazi hao zinaendelea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment