Wednesday, 20 February 2013

KATIBU MKUU WA BARAZA LA MITIHANI ADAI CLOUDS FM IMECHANGIA UANDIKAJI WA MATUSI KWENYE MTIHANI YA FORM 4 MWAKA HUU...!!!Katibu mkuu wa baraza la mitihani la taifa, Bi Joyce Ndalichako, amekilaumu kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa kilimpa promotion kijana aliendika matusi na "Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.

Katibu mkuu huyo amedai kuwa hatua hiyo ya Clouds FM imechangia uandikaji wa matusi kwa watahaniwa wa mwaka huu.

Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.

Source: Clouds FM asubuhi ya leo.

No comments:

Post a Comment