Sunday, 17 February 2013

Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya kuuwawa kwa Padri Evaristitus MushiPadri Evaristitus Mushi

Padri Evaristitus Mushi wa KANISA la katoliki,Parokia ya ST.Joseph,Shangani,Unguja ameuwawa leo mnamo saa moja asubuhi katika eneo la Beit-EL-Ras karibu na kanisa la Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mohamed Aboud imeeleza kuwa kutokana na tukeo hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatambua wale wote waliohuka na tukio hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria.

Aboud amesema kuwa wakati uchunguzi huo unaendelra, Serikali inawaomba wananachi wote kuwa watulivu na kuliachia Jeshi hilo la Polisi kutekeleza wajibu wake .

Aidha Serikali imetoa mkono wa pole kwa familia na wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment