Monday, 18 February 2013

WAUZA BANGE NA UNGA WAMERUKIWA JANA SEBULENI VASA BAR

vasa raid

habari zaidi bofya www.svt.se/nyhetsklipp/regionalt/abc/article1019963.svt

jana ilikua kitim tim pale sebuleni kwetu kwa zamani ambapo polisi walifika ghafla na vingora na kuzingira eneo hilo,baada ya kuzama ndani ya bar wakawafuma wa-west kama kawaida yao wakiuza ndumu kama njegere.kwa jinsi walivyokuwa wamejisahau mmoja amekutwa kaanika kete za unga na bangi mezani na waala hana wasi wasi anasubiri wateja.mwingine alikimbilia chooni walipomkuta nae ana bange kibao kwenye jacket
polisi wamesema walikua wanafatilia kwa muda wa wiki mbili na kuona kinachoendelea,na hivyo jana wakaamua kuangusha ambush.jamaa waliodandiwa kama kawaida watafikishwa mahakamani na kupumzishwa hotelini(jela ya mswed hotel kwa maganga) pale sollentuna kwa miaka kadhaa.

imekua kawaida kwa bar hii ya vasa watu kugeuza ndio kijiwe cha kuuza vitu vya wizi na madawa ya kulevya.hii si mara ya kwanza kwa polis kuvamia maeneo yale.kipindi cha nyuma ilikua inatokea sana mpaka waafrika wengi ikabidi tupunguze mahudhurio maeneo hayo maana ulikua unaweza kujikuta uko kipawa huku ukiangalia mabati mekundu yenye kutu ya bom bom kiembe samaki wakati unakaribia kutua na ndege ya mswede.

No comments:

Post a Comment