Wednesday, 27 February 2013

VIROJA MADE IN SVERIGE!

Top prosecutor nabbed in prostitution sting

haya haya leo tena tunawaletea vimbwanga vinavyoendelea hapa.
jana katika msako wa polis hapo mjini hotelini moja inayofahamika kwa kuuza makahaba.kimezuka jambo ambalo limekuwa kioja kinachoongelea sana hapa.hiyo ni pale polis katika kufanya msako wao na kufatilia kwa muda mrefu wakaamua wakatege mingo ili wamkamate kahaba japo mmoja tu akiwa na mteja wake.
polis hao wakatega mingo zao kwenye ngazi baada ya kuona kwa mbali katika microscope zao kwamba kuna mteja kaingia chumbani kwa kahaba.
baada ya kusubiri kwa muda mreefu sana mara jamaa akatoka ndani akiwa tayari kashakamuliwa wale wadudu.jamaa baada ya kutoka ndani ya room  hamad polis wakamshtukiza"uko chini ya ulinzi"
yule bwana akanyosha mikono juu kuashiria kasalimu amri.
kichekesho na kiroja kinakuja wapi? ni pale polis walipotambulishana na kugundua kuwa kumbe jamaa waliyemkamata ndio hakimu ambaye walikuwa wanamtegemea sana kusimamia kesi kama hizo za makahaba.na hata hapo walipoenda kutega walikua wanasubiri wakikamilisha uchunguzi wampelekee yeye kesi.
sasa kesi ya nyani umpelekee nyani sijui itakuwaje.huyo bwana amekiri kwamba ndio alienda kufanya ngono na hajali,mke wake na watoto waliposikia akabwaga manyanga.wakili huyo hajutii kitendo hicho anasema tu ndio nimeenda na wamenikamata poa.
 imebidi polis wamtafute hakimu mwingine ili asimamie kesi hiyo.
habari zaidi bofya HAPA

NB
KUANZIA SASA TUTAKUA NA KITENGO HIKI CHA VIROJA MADE IN HAPA HAPA,BADO TUNAENDELEA KULA NYAMA YA FARASI TUKIMALIZIA TUTAWAMWAGIA MASTORO HAPA INA LADHA GANI.

KAMA UNA KIROJA MDAU USISITE KUTUTUMIA 

No comments:

Post a Comment