Wednesday 13 November 2013

Kontena lenye meno ya tembo limekamatwa Unguja

Kontena lenye urefu wa futi 40 lililojaa pembe za ndovu limekamatwa kisiwani Unguja mchana huu likitokea bandari ya Dar es Salaam.

Mpaka sasa haijajulikana mzigo huo una thamani ya kiasi gani na raia wawili wa Tanzania wamekamatwa kuisaidia polisi .
Kwa mujibu wa Waziri Kagasheki, kontena hilo pia linahisiwa kumilikiwa na raia wa China.

Tukio hilo limeshudiwa na Waziri wa nchi tawala za mikoa Zanzibar pamoja na Waziri wa maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki.

Source: Eatv/ Radio

No comments:

Post a Comment