Tuesday, 26 November 2013

Yaliyojiri Show ya P-square Bongo

Stori:  Erick Evarist na Musa Mateja
UJIO wa wanamuziki mapacha, Peter na Paul Okoye ‘P –Square’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa! Anga la burudani la Bongo limetikisika na kuzua gumzo kubwa, Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matukio muhimu.
Peter Okoye akim-kiss Beautiful Onyinye wake wa Bongo.

Wanamuziki hao walitua Bongo na kufanya shoo kubwa Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar kwa kusindikizwa na wasanii wa nyumbani, John Saimon ‘Joh Makini’, Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na Bernard Paul ‘Ben Pol’.
...Akimkumbatia Beautiful Onyinye wake.

Kabla ya kutua nchini, wasanii hao maarufu zaidi Afrika, walikuwa wakizungumzwa hususan Peter ambaye hakuwa na muda mrefu tangu atoke kufunga ndoa ya kimila nchini kwao, Nigeria.
Ndoa yake ilizua mjadala, kila mmoja alitaka kujua maisha yake baada ya ndoa lakini mkazo zaidi uliibuka jukwaani pale alipompandisha binti wa Kitanzania na kumtambulisha kama mkewe wa Bongo.
Mrembo akinyoosha mkono avishwe saa na Peter.

ILIKUWAJE?
P-Square wakiwa kwenye morari ya shoo, saa 6 na nusu usiku, walilivamia jukwaa na kuanza kutumbuiza nyimbo zao kali zilizoshangiliwa na mashabiki kuanzia pale walipoanza kuimba wimbo wa kwanza.
...Akivishwa saa ya bei mbaya.

Waliimba wimbo wa Temptation, Danger, E No Easy na nyingine kibao lakini ilipofika wakati wa wimbo wa Beautiful Onyinye, mambo yaligeuka kidogo.
Peter aliona kuna haja ya kumpandisha mrembo wa Kitanzania na kumtangaza kuwa ni mkewe wa hapa Bongo.
Petere akisimamisha shoo baada ya Beautiful Onyinye kupanda stejini.

ASIMAMISHA SHOO
Peter aliusimamisha wimbo huo wa Beautiful Onyinye usiendelee kurindima na kumtaka mrembo yeyote anayehisi kwamba ana sifa za kuwa Beautiful Onyinye (akimaanisha katika wimbo wao uitwao hivyo) apande jukwaani.
MREMBO AIBUKA
Kwa mwendo wa maringo, ‘dada’ yetu wa Kibongo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, aliwaacha marafiki zake waliokuwa wakifuatilia shoo hiyo na kupanda jukwaani.
Peter akiongea na mrembo huyo.

Peter alipomuona mrembo huyo alidata kutokana na mwonekano wake wa kuvutia, aliamuru muziki usimamishwe kwa muda ili azungumze naye mawili matatu, dada yetu ambaye alionekana kujawa na aibu za kike, alimtazama Peter kwa bashasha huku akimshushia tabasamu mwanana.
PETER AFUNGUKA
Baada ya kusimama naye kwa muda, Peter ambaye pia alionekana kupagawa na mrembo huyo, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa akitafakari cha kufanya, baada ya muda akaona isiwe tabu, akafunguka:
“Jamani kila mmoja wenu anatambua kuwa hivi karibuni nimeoa kule kwetu Nigeria, lakini niwe mkweli huyu ndiye Beautiful Onyinye wa Bongo. Nimeoa Nigeria lakini sasa huyu atakuwa mke wangu wa huku Tanzania, atakuwa mke wangu wa pili,” alisema na kushangiliwa kwa nguvu.
‘SINI’ YA MALAVIDAVI
Peter aliyekuwa akitazamwa na maelfu ya mashabiki waliofurika, alimtaka mrembo huyo kunyoosha mkono wake wa kushoto, akatafakari kidogo kisha akavua saa yake na kumvisha  kama ishara ya upendo.
Kitendo hicho kilienda sambamba na shangwe za mashabiki ambao walikuwa wakiamini kuwa Peter alikuwa amepagawa kimalavidavi kwa mrembo huyo.
Aidha wengi walidhani Peter amemvisha pete ya uchumba au ndoa  mrembo huyo wakawa wanajiuliza kulikoni?
Peter aliwakata maini zaidi Wabongo baada ya kummiminia mabusu motomoto mrembo huyo kisha akamruhusu  kushuka jukwaani.
Hata hivyo, mrembo huyo aliposhuka jukwaani, alilakiwa na mashostito wake ambao walikuwa wakitamba kwamba wamemfunika Wema Isaac Sepetu ambaye alikuwa akijiita Beautiful Onyinye wa Bongo.
SHOO INAENDELEA
Baada ya kumalizana na mrembo huyo, P–Square walizidi kuporomosha nyimbo zao huku wakifuatishwa na mashabiki waliopagawa kwa nyimbo zao. Vijana hao watanashati waliimba kwa hisia, sauti zao zilitoka vizuri.
Mchanganyiko wa vyombo vya bendi na CD ulisikika vizuri, wakaendelea kuwapagawisha Watanzania.
Katika kunogesha shoo yao, P- Square walionesha uwezo wa kutumia vifaa mbalimbali vya muziki kama magitaa na ‘drums.’
Kama vile haitoshi, kuna wakati wasanii hao walinogesha shoo yao kwa kushindana kuonesha miili yao jinsi ilivyojengeka vizuri na kuwaacha hoi wadada wa Kibongo waliokuwa wakitamani hata kuwagusa.
Peter alivua shati na kuonesha kifua chake huku Paul akimjibu kwa kuvua suruali yake na kubaki na boxer (kama alivyofanya Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati wa Tamasha la Fiesta la mwaka jana).
Hadi kufikia saa 9 usiku, wasanii hao walikuwa bado na uwezo wa kuendelea na kazi kwa kuwa walikuwa na pumzi za kutosha.
Hatimaye wakawataka mashabiki kuchagua nyimbo wanazopenda zirudiwe, nyimbo zilizopendekezwa ni Chop my Money na Personally. Bila hiyana walizirudia hadi mashabiki waliporidhika.
SOMO
Wasanii wa nyumbani wanapaswa kujifunza kupitia shoo hiyo, kulikuwa na tofauti kubwa sana ya sauti kusikika vizuri katika shoo ya P-Square na pale wasanii wa nyumbani walipokuwa wakitumbuiza. Wasanii wa nyumbani hawakuwa wakisikika vizuri.
TURUDI KWA BEAUTIFUL ONYINYE WETU
Mpaka shoo hiyo iliyokonga nyoyo za wapenzi wengi wa muziki ilipofikia mwisho, haikufahamika mara moja kama binti huyo ‘Beautiful Onyinye wa Bongo’, aliondoka na Peter au mchezo uliishia juk
waani.

No comments:

Post a Comment