Saturday, 28 December 2013

BINTI MREMBO WA KITANZANIA ADAKWA NA MADAWA HUKO MACAU
Polisi wakichunguza vidonge ambavyo huyu mrembo alikuwa amevimeza. 
Waandishi wa habari wakipiga picha vidonge vya heroin alivyokamatwa navyo mremboi huyu wa Kitanzania.Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.

chanzo.JF

ISAACKINWELL,MPAKA SASA HABARI ZILIZOPO NI KWAMBA BINTI HUYOI NI JACK CLIFF MODO AMBAYE ALIOLEWA KWA MBWEMBWE NYINGI NA BAADA YA MIEZI KADHAA MUMEWE AKAKAMATWA NA HAYO MAMBO YA MADAWA MKE AKATOSA NA KUTOKA BARU.INASEMEKANA PIA WALIKUA PAMOJA NA YULE BINTI KIZIWI HUKO CHINA ALIPOKAMATWA NA UNGA.HAYA HIVI SASA NDIO KAMA AROBAINI YAKE ILIFIKA.
BY THE WAY TUMEONGEA NA KUZUNGUMZA SANA HII ISSUE WENGINE TUKAAMBIWA "UOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO".

INACHEKESHA KWANI VIJANA WANAOIBUKA HIVI SASA WAKATI HUU KUFANYA HIYO BIASHARA NWAMEKUWA MALIMBUKENI,KILA SIKU KUJITANGAZA TANGAZA VIPESA VIDOGO WANAVYOPATA KWA BIASHARA HIYO,WAO LEO WANAONA UJANJA WAKATI WENZAO WALIPIGA BIASHARA MIAKA HIYO TENA KIMYA KIMYA NA HAKUNA KTU KUSIKIA AMEKAMATWA.
SASA HIVI BASI MTU AKIFANIKIWA KURUSHA MZIGO AKANUNUA KAGARI INSTA NA FCBK WATAMKOMA.KWETU HAPA SVERIGE NDIO IMEKUA BALAA VIJANA KIBAO WAMEPOTEA HATUWAONI KITAA UKIULIZA UNAAMBIWA WALIBEBA MADUDE WAKADAKWA.HIYO NDIO TABU YA KUTOKUWA NA ELIMU,MTU ANABEBA VITU HARAMU NA KWA UMBULULA WAKE ANADHANI HAPA ULAYA UTAPASUA KILAINI,UMEKUJA MTONI KIAJABU AJABU BADALA YA KUDANGANYA SIJUI WE MKIMBIZI SIJUI MSOMALI MNAJUA WENYEWE,BAADA YA KUPEWA SHERIA MNAKIMBILIA KWENDA KUFANYA UPUNDA NA HUKU OPPOTURNITY ZIPO KIBAO.

BAADA YA HAPO UNAISHIA KUFUNGWA NA UKIWA KIFUNGONI JAMAA NDIO WANAINGIA IN DEEP KUFAHAMU ORIGINALY YAKO,HAPO UKITOKA NI ONE WAY TRIP TO BONGO UKAANZE MAISHA MAPYA.
 ANYWAY NYIE ENDELEENI TU KUBURUTA SIE TUNAENDELEA KUWAHESABU TU MPAKA MUISHE WOTE HUKU MITAANI TUACHE KUBANANA

ALAMSIKI

No comments:

Post a Comment