Thursday, 12 December 2013

ISAACKIN NDANI YA LIBENEKE 24/7 TENA


Maganga mimi nikijaribu kuparura samaki kama mvuvi pale ziwa viktoria

habari za masiku waungwana na wanakijiwe hiki cha Isaackin.ni masiku kibao nimekuwa sipo hewani kwa muda mrefu japo nilikuwa busy sikuwasahau kwa kuwatundikia habari za hapa na pale zinazoendelea ulimwenguni.
ingawa mlinikosa kwa habari zangu moto moto na zingine za kuchefua akili kwa sasa kijana wenu mtiiiifuuuuuuuu,mwaminiiiiiiifuuuuu,nkonyofuuuuu(km mnakumbuka kale kababu kanapuliza chai ipoe)ok  niko hewani tena.
kwa ujumla nilikua nimeingia ile elimu ya ukubwani kujaribu kutoa ujinga maana sometyme akili unaifeel ikiwa matope matupu.na kwa sisi tuliokuja zamia nchi za wenyewe bila shule kuna kupiga deki na kifagio kinakusubiri mpaka ufe.
otherwise ni kusoma tu huku hamna kukimbia umande.kwasababu umande tunaishi nao na wenyewe wenye nji yao hii wanaupenda umande utaukimbia uende wapi?sometyme ni kama tunameza chai yenye pilipili kibao huku tukiisifia ina utamu wa asali.
haya bandugu kwa sasa nimerudi mtaani kama kawaida na tuendeleze libeneke kwa kutumiana mapicha ya bethedei,kumeremeta,michango ya harusi,misiba(hii si sana).komunyoo n.k.

No comments:

Post a Comment