Thursday, 19 December 2013

Majanga ya kibongobongo.


Mama kajitwika lita 20,mtoto nae hayuko nyuma,angalau ana japo lita moja ya Maji toka kopo la kimbo.
Hii ni hali halisi ambayo wengi wao tuliipitia enzi za njaa,kwasasa nani anakumbuka.kila mtu anajifanya mtoto wa kishua kisa yuko ulaya.
Kwa ujumla mi shuhuli hizi huwa nazifanya kila mara nnapokua home umagangani.kule habari ya advertise sijui nimetoka mtoni huwa naisahau kwa muda.tunakuwa wote wanakijiji.

Tatizo linakuja mtu unatoka Ulaya status ya ukimbizi,haya umekusanya kanauli mwaka Mwaka mzima,ukakusanya kahela ka matumizi mwaka mwingine.na kukusanya si kukusanya(ni kupiga deki,kusugua masufuria,kufagia vyoo na zinazoendana na hizo.
Baada ya hapo huyu mshua akishuka bongo basi anataka kula bata kutembelea ma VX ya washkaji bila kushtuka kwamba huku fagio linamngoja.
Mtu akinunua  viraba vya rea kr 300 tajiri yeye,mtu akienda club ya kueleweka tajiri yeye,mtu akienda kula lunch kitu ambayo kwa kipato cha Hapa ni kawaida lakini maganga ni sikukuu.kuna mabwege wengine watathubutu hata kukuonyesha maziwa na cheese na soda zilivyojaa kwenye friji,maganga huyo anakwambia anakula bata,hallooooow!
Tuko huku jamani kilomita elf 11.maisha haya mkijaribu kufananisha na yaleeeeee,ndo zinakuja habari hizo za kukaa tu na kungoja sociale wakupe senti yao ukale,kisa we mkimbizi.
Amka,Jiamshe,Shtuka,Tupa blanketi ingia mitaani ukatafute maisha.
Maisha si kula ugali na vibawa,hons,sambusa
Maisha si kucheza ndombolo ya dekula
Maisha si kununua kiatu au Nguo nzuri
Jiulize whats your future here??will you Continue to lie till you die??
If you think you Will get a lot of free money one day forget it "no free lunch in Sverige"

The only advice is to wake your ass upp and go to work
Thats where respekt comming from.



1 comment: