Monday 3 March 2014

BILIONEA SHKUBA ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA DAR

BILIONEA maarufu jijini Dar es Salaam, Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) ambaye alikuwa akisakwa kwa muda mrefu na Kikosi Maalum cha Polisi Tanzania kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya ‘unga’, amenaswa.


Bilionea Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) aliyenaswa na polisi.

Vyanzo vililiambia gazeti hili kwamba, mtuhumiwa huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Februari 23, mwaka huu, saa sita mchana akijianda kwenda nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mara baada ya Shkuba kukamatwa alisafirishwa usiku huohuo kwenda mkoani Lindi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo Februari 27, mwaka huu aliunganishwa na watuhumiwa wengine na kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Kusini.

Click image for larger version. 

Name: Pipi2000.jpg 
Views: 0 
Size: 74.9 KB 
ID: 142645



Madawa ya kulevya.


Shkuba ambaye ni mkazi wa Mikocheni, Dar ni mfanyabiashara mwenye maduka ya kubadili fedha (bureau de change) jijini, ana makampuni ya ulinzi na nyumba Mikocheni pia anamiliki magari ya kifahari likiwemo aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150.


Vyanzo hivyo vilisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisakwa na kikosi kazi tangu Januari 12, 2012 na inadaiwa kwamba alikimbilia nje ya nchi na kurudi kwa siri na ndipo jeshi hilo liliamua kumuwekea mtego.

Taarifa ziliendelea kusema kuwa, tangu vita ya kuididimiza biashara ya unga ianze nchini, hakuna bilionea aliyewahi kukamatwa zaidi ya mtuhumiwa huyo.

Click image for larger version. 

Name: pipi20000.jpg 
Views: 0 
Size: 71.4 KB 
ID: 142646

Gari aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya milioni 150 ambalo ni mojawapo ya magari ya kifahari anayomiliki Shkuba.



Vyanzo vingine vya habari toka ndani ya jeshi hilo vinadai kwamba, Shkuba aliwahi kukamatwa mwaka 2006 kwa kuhusishwa na biashara hiyo haramu na kuwekewa ulinzi wa kifungo cha nje.



Habari zinadai kuwa, Januari 12, 2012, kikosi kazi cha kupambana na biashara hiyo kilipata taarifa ya kuwepo kwa madawa hayo aina ya heroin kiasi cha kilo 211 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 mkoani Lindi yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi.



Kikosi hicho kiliweka mtego maeneo ya Machinga Two mkoani humo na kufanikiwa kukamata unga huo uliokuwa umefichwa katika hoteli moja.


Click image for larger version. 

Name: pipi200000.jpg 
Views: 0 
Size: 44.5 KB 
ID: 142647


Binti wa Liyumba, Maureen Liyumba, siku alipokamatwa pamoja na wenzake wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 mkoani Lindi yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi.



Watu wanne walikamatwa sanjari nao, akiwemo binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, Maureen Liyumba ambaye yuko mahabusu mpaka sasa na ameungana na Shkuba.



Vyanzo hivyo vilidai kwamba watu hao walikuwa wakiwasiliana na Shkuba ambaye watuhumiwa walimtaja na ndipo polisi walipoanza kumfuatilia.


Click image for larger version. 

Name: pipi200000000.jpg 
Views: 0 
Size: 48.8 KB 
ID: 142648


Madawa ya kulevya aliyokamatwa nayo binti wa Liyumba na wenzake.



Siku moja nusura polisi wamkamate ambapo alikimbia na kulitelekeza gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T921 BPY ambalo bado linashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Lindi.



Inadaiwa kwamba polisi walipokwenda nyumbani kwake jijini Dar walimkosa na kila walipopiga simu zake zilikuwa hazipatikani hewani lakini baada ya kumkamata walimpeleka Lindi kwa helikopta.



Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi na Uwazi kuhusu madai hayo alithibitisha kukamatwa kwa Shkuba na kwamba tayari ameunganishwa na wenzake mkoani Lindi na wanaendelea kuwasaka mabilionea wengine ndani na nje ya nje ya nchi.



Click image for larger version. 

Name: pipi343.jpg 
Views: 0 
Size: 54.7 KB 
ID: 142649


Maureen Liyumba pamoja na watuhumiwa wenzake.



“Ni kweli tulikuwa tukimsaka kwa muda mrefu Bwana Shkuba na tulijipanga vizuri sisi kikosi kazi hali iliyotufanya tumnase.



“Hii vita ya biashara haramu kwa sasa si kwa Tanzania tu bali ni vita ya dunia nzima, nawaomba wananchi wazidi kutupa ushirikiano na tutayafanyia kazi kwa siri maelezo yao,” alisema Kamanda Nzowa.




source; Global Publishers

No comments:

Post a Comment