Sunday, 1 June 2014

SIKU YA KISWAHILI 7 June 2014, StockholmKwa Jumuia ya Watanzania,

Mnakumbushwa ukaribisho wa kuhudhuria Siku ya Kiswahili itakayofanyika tarehe 7 June 2014 katika ukumbi wa Bergshamra Skola, Hjortstigen 1, Bergshamra, Solna. Shughuli hii itaanza saa 7.00 kwa chakula cha mchana. 

Kwa wale wenye bidhaa za kuuza au kuonyesha wanakaribishwa kufanya hivyo. Toa taarifa kwa Bw. Osore Ondusye 0736350189 ili aweke meza na wahi katika ukumbi saa 6.30 mchana.

Kipeperushi kwa ajili ya shughuli hii kimeambatanishwa.

Ukipata taarifa tafadhali mwarifu na mwingine.


Jacob Msekwa
kny: BALOZI

No comments:

Post a Comment