Friday, 29 January 2010
VIDEO>BEN AELEZA ALICHOKIONA USIKU WA MAUAJI YA SWETU
inatia uchungu sana lakini sielewielewi hawa jamaa kwanini walikuwa busy sana kumshughulikia marehemu,kama ben anavyosema kwamba walimtrick kama wanaenda o,bay kisha wakapotelea mitaani kwenda kuendeleza umafia wa kumfanyizia jamaa basi lazima kuna kitu kimejificha hapo si bure.
Thursday, 28 January 2010
WALIOPORA UHAI WA SWETU HAWA HAPA MAHAKAMANI
ningeshukuru sana kama nawao wangenyongelewa mbali basi angalau tupunguzehasira,lakini kwa bongo mmh,usije shangaa ikaundwa tume kufanya uchunguzi,miaka miwili badae ukaambiwa waliuwa bila kukusudia,halafu wakahukumiwa mwaka mmoja,then baada ya miezi mitatu wakachiwa kwa msamaha wa rahisi,bongo sheria kizungumkuti tu
Wednesday, 27 January 2010
R.I.P SWETU FUNDIKIRA
WA KARIBU KAULIWA KINYAMA PASI KUWA NA SABABU YOYOTE YA MAANA,NASHINDWA KUELEWA NINAPOSIKIA HAWA WAJESHI WAMEMTOA ROHO RAFIKI ETI KISA KAKWARUZA GARI LAO,HIVI INAINGIA AKILINI KWELI?BONGO
INATIA UCHUNGU SANA NA KUHUZUNISHA PALE UNAPOSIKIA RAFIKI NA MTU WAKOKUPIGANA PASI MBONA KAWAIDA TU MNAELEWANA MNAMALIZANA HAPOHAPO SASA NININI HIKI?UTAMUUAJE MWENZIO ETI KWAAJILI YA KUCHUNA GARI YAKO?IMENIUMA SANA KWAKWELI,KWA UPANDE MWINGINE NINGEWEZA HATA KUELEWA KAMA MAREHEMU SWETU ANA HISTORIA YA UGOMVI AU DHARAU,JAMAA ALIKUWA MTU POA SANA MTARATIBU NA SIKU ZOTE AKISISITIZA USTAARABU,HATA SIWEZI KUAMINI UKINIAMBIA ALIWAJIBU VIBAYA AU KUWATUKANA,NO NAKATAA KWANI MIAKA KUMI NA KITU NILIYOMJUA SIKUWAHI KUONA HATA AKIMDHARAU MTU ACHILIA MBALI KUTUKANA,KWELI BONGO MAISHA YAKO REHANI HAKYANANI,HAYA YAKUTOKEA YAMETOKEA TUNAMUOMBEA MAREHEMU APUMZISHWE KWA AMANI NA MUNGU ABARIKI NDUGU NA FAMILIA YA MAREHEMU,AMINA
N:B,USHAURI SERIKALI IWAJENGEE WANAJESHI BARABARA ZAO BWANA MAANA SASA VIFO VITAONGEZEKA NA VILEVILE KILA MJESHI ANAPOKUA BARABARANI NA GARI YAKE AWEKE ALAMA ILI WATU WAWE WAANGALIFU WAKAE MBALI WASIJE KUTOLEWA UHAI WAKIIGONGA AU KUIPIGA PASI GARI YAKE.
Monday, 25 January 2010
Nine bodies found from Ethiopian Airlines crash
Beirut, Lebanon (CNN) -- Rescue crews searched feverishly in poor weather conditions Monday for passengers from an Ethiopian Airlines flight that crashed into the Mediterranean Sea minutes after takeoff with 90 people aboard. By Monday morning, crews had found nine bodies, but no survivors, off the Lebanese coast where the Boeing aircraft had gone down, the Lebanese government said. Prime Minister Saad Hariri announced a day of mourning for the victims of the crash, ordering all government departments to close, the national news agency reported. He praised security forces and the Red Cross for their efforts in the aftermath of the accident. Ethiopian Airlines Flight 409 left Rafik Hariri International Airport in Beirut about 2:30 a.m. and was headed to the Ethiopian capital, Addis Ababa. It disappeared from radar a few minutes after takeoff, said Ghazi El Aridi, Lebanon's minister of public works and transportation. Authorities did not immediately know the cause of the crash. "We don't believe that there is any indication for sabotage or foul play," Lebanese President Michel Sulayman said. habari hizi za kusikitisha zimefika asubuhi hii,mungu awabariki marehemu ambao mpaka sasa ni kumi na nane(18)
Friday, 22 January 2010
FALLY IPUPA ZENITH JAN 2, 2010
kama nilivyoahidi show hiyo hapo ni moto mkali vibaya jamaa wanapiga uno kama wamepagawa show imetulia na nyimbo zina mpangilio,sijaona kung fu style wala sarakasi humu ni show la kufa mtu wadau pateni utamu.
Thursday, 21 January 2010
HARUNA MOSHI*BOBAN*ATUA SWEDEN
Don't be fooled by Mtagwa's record!
Don't be fooled by Mtagwa's record"Rogers Mtagwa doesn’t have the backing of a high-profile promoter or an influential manager. Nor does he have a television network clearing dates to broadcast his fights. He doesn’t have his own publicist. He’s rarely, if ever, called out by anyone.
He operates far from the spotlight that shines so brightly on guys like Floyd Mayweather Jr., Manny Pacquiao and Shane Mosley. He speaks next to no English and can’t plead his own case, like a Mayweather does so effectively. He struggles to get by on his boxing income, so much so that he still goes to work as a roofer, weather-permitting, in his adopted hometown of Philadelphia.
Yet, know this: Miss a Mtagwa fight at your own peril.
For all the things he’s not, for all the things he doesn’t have, he does have this: A fighting spirit unsurpassed in professional boxing."
ingawa hana record nzuri lakini naona jamaa anakubalika maana jamaa anaitwa(MOYO WA SIMBA) si mchezo,na kinachofanya wamkubali ni uwezo wake wa kuvumilia na kupigana raundi zote bila kukata tamaa na ndiyo inavyotakiwa,endelea na moyo huo MTAGWA iko siku nawewe utaweka historia ya TANZANIA juu.
Wednesday, 20 January 2010
RAIN BOW AU UPINDE WA MVUA
zamani tulisimuliwa hadithi nyingi sana juu ya hii kitu,lakini sijui kama ni kweli ingawa mnimi nnachoona na kufurahia hapo ni huo uzuri wa picha uliotukuka
source:mjengwa.blogspot.com
source:mjengwa.blogspot.com
Tuesday, 19 January 2010
Friday, 15 January 2010
MAPISHI YA PWANI:BIRIYANI YA NYAMA.
VIPIMO VYA NYAMA
Nyama 2 Ratili (LB)
Chumvi kiasi
Mafuta 1 Kikombe
Samli ½ Kikombe
Kitungu (Kata virefu virefu) 3 Vikubwa
Nyanya (kata vipande) 2
Nyanya kopo 1 Kijiko cha chakula
Thomu 1 Kijiko cha chakula
Tangawazi 1 Kijiko cha chakula
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Pilipili ya unga nyekundu ½ Kijiko cha chai
Kotmiri iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula
Viazi 6
Gram masala 1 Kijiko cha chai
Mtindi ¼ Kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA
1. Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.
VIPIMO VYA WALI
Mchele 5 Magi (Kikombe kikubwa)
Hiliki nzima 4
Mdalasini mzima 1
Zafarani ½ kijiko cha chai
Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe
Chumvi kiasi
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
3. Tia hiliki na mdalasini.
4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
6. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
7. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.
source:alhidaaya.com
KITCHEN PARTY BONGO MMH!
ndio maana wanaume hatuitajiki kwenda kama mambo yenyewe ndo haya mzuka unaweza ukupande ghafla mwananchi ukamrukia mtu maana mmmh!waende wenyewe sawa tu.
Thursday, 14 January 2010
TIGER WOOD NA MAKASHESHE YAKE
TETEMEKO LA ARDHI HAITI JAN 13
MAOMBOLEZO YA SIMBA WAVITA STOCKHOLM SWEDEN
Friday, 8 January 2010
LEO BIRTHDAY YA KANUMBA THE GREATEST
PAMBANO LA FLOYD MAYWEATHER NA PAQUANO LAAHIRISHWA
pambano hilo la uzito wa welterweight limeahirishwa baada ya floyd kutaka jamaa achukuliwe vipimo vyoote,hadi ngoma kabla hajaingia ulingoni,na jamaa nae akasema ana matatizo ya woga wa kuchomwa sindano hivyo akichukuliwa vipimo ataathirika akiingia ulingoni,pambano ambalo lilikua liwaingizie midola ya kufamtu limefutwa.sasa changamoto kwa mabondia wetu hapo nyumbani sijui itakuwaje hii sheria ikiingia maana juzi nimeona picha tubondia fulani tunapima kwa ajili ya mpambano nikachoka,hata kama wanapigana uzito mdogo afya yao ilikua mgogoro kwakweli,yaani washauriwe wapige msosi na tizi halafu wawe wanacheki afya mara kwa mara vilevile.
Thursday, 7 January 2010
OLD IS GOLD WENGE B.C.B.G 4X4 1989
enzi hizo wenge wakitesa na vibao vyao kama djino,dady bitodi,nick d,kipindi hiyo unawakuta manda chante,alain mpela werrason,didier masela,alain makaba,marie paul,na wengine wengi tu wadau mnaweza kumalizia hapo,yaani enzi hizo ilikua balaa style ni bon chik bon gere,moto mkali,hapo JB hakuwepo.
FALLY IPUPA AKIFANYA MAZOEZI KABLA YA KUACHIA SHOW YA KUFAMUTU PARIS
show live yenyewe nzima ntaweka hivi punde,ngoja mwakilishi wangu aliyekuwepo kwenye show anirushie mtaziona hapahapa.tuwe pamoja
RIHANNA NA BOYFRIEND MPYA TENA
Hapo ndo utakoma na mademu,maana wanakomaa nasi kichizi,ukileta kuringa anatambaa sikumbili tatu unamkuta na jamaa mwingine,sasa ndo utajua ujinyonge au uamue uwe mlevi basi yaishe,maana unapomwacha sometime inakua unatingisha kiberiti mwenzio anafanya kweli,halafu jamaa wanaokuwa wamemiliki baada ya hapo wanakuwa wakali kweli wanakaba mpaka golini
MAMBO YA MASEBENE KAMA KAWA TUNAWAKILISHA
DA!NIMEMISS SANA HAYA MAMBO PALE MANGO GARDEN
Wednesday, 6 January 2010
MITANDAO IMEINGILIWA NA WAPUUZI?
SIKU HIZI MITANDAONI IMEKUA SOO TUPU MAZEE,YAANI HAWA WANAIJERIA WANATUNYANYASA SI MCHEZO MAANA SASA TUNASHINDWA HATA PA KUTOKEA,JAMAA WALIFANIKIWA KUCHOTA PASSWORD YANGU MAHALI,BASI WAKANIFUNGIA MAIL NIKAWA NASHINDWA KULOG IN,SASA KILICHOTOKEA BADO WANAENDELEA KUNIFATILIA KILA MAHALI,BLOG YANGU INGINE IMEBIDI NIFUNGE KWANI SIWEZI KULOG IN MAIL ILE NILIYOFUNGULIA NDIO WANAYO KILA NIKIJARIBU WANANAMBIA MPAKA ADMIN AVERIFY WAKATI ADMIN NI MIMI MWENYEWE,NIKIENDA KULE KWENYE MAIL NYINGINE NILIYOBADILISHA SIONI MAOMBI YA KUVERIFY BLOG MEMBER BALI WANANTUMIA FOMU ZINGINE NIJAZE PASSWORD NA EMAIL HAPO NDO NASHANGAA SASA,LAKINI HAYA MAMBO YA KUTAPELIANA YATAENDA MPAKA LINI SASA???
MAMBO NATURAL*mama yeyoo*MMH
INTRO (MNAKARIBISHWA)UKUMBINI
karibuni waungwana kwenye kiwanja chetu hiki cha burudani,hapa utapata music,video,picha za matukio ya kila aina hasa michezo,kwa ujumla burudani ya aina yoyote ile,popote pale itawekwa hewani,vilevile mnakaribishwa kutuma maoni,picha za burudani kutoka mahali popote duniani zitawekwa mradi si matusi wala kashfa,picha kutoka kwenye kumbi yoyote ya starehe hasa bongo zinakaribishwa nami ntajitahidi kuwawekea chochote ntachokipata,haya wakubwa tushirikiane kunogesha jukwaa letu hili,ahsanteni
Labels:
utambulisho
Subscribe to:
Posts (Atom)