Sunday, 9 June 2013

MASHUJAA BAND, KALA JEREMIAH, OMMY DIMPOZ WAIBUKA VINARA TUZO ZA KILI 2013

Mshindi wa tuzo tatu, Kala Jeremiah akiwa na moja ya tuzo zake.
Chalz Baba akipokea moja ya tuzo zake kutoka kwa Mtangazaji Maulid Kitenge. Chalz alishinda tuzo mbili na kupokea tuzo nyingine mbili kwa ajili ya bendi yake ya Mashujaa.…
Mshindi wa tuzo tatu, Kala Jeremiah akiwa na moja ya tuzo zake.
Chalz Baba akipokea moja ya tuzo zake kutoka kwa Mtangazaji Maulid Kitenge. Chalz alishinda tuzo mbili na kupokea tuzo nyingine mbili kwa ajili ya bendi yake ya Mashujaa.
Mshindi wa tuzo tatu, Ommy Dimpoz akipokea moja ya tuzo zake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kushoto) akimpatia Amoroso tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Wimbo wa Mwaka wa Bendi.
Henry Mdimu akimkabidhi Amin tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba.
Mmiliki wa Zizzou Fashion, Tippo (kulia) akitoa tuzo kwa Rappa Bora wa Bendi, Ferguson.
Luiza Mbutu akipokea tuzo yake ya Msanii Bora wa Kike - Bendi.
Mwenyekiti wa African Stars 'Twanga Pepeta' Baraka Musilwa (kulia) akimkabidhi tuzo Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid a.k.a Suma kwa niaba ya Isha Mashauzi.BENDI ya Mashujaa, Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wameibuka kidedea kwa kutwaa tuzo nyingi kuliko wasanii  na bendi nyingine kwenye sherehe za utoaji tuzo za Kilimanjaro. Bendi ya Mashujaa pamoja na wanamuziki wake wametwaa tuzo tano ambazo ni Bendi Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Kiswahili - Bendi, Rappa Bora wa Bendi ambaye  ni Ferguson, Msanii Bora wa Kiume - Bendi na Mtunzi Bora wa Mashairi - Bendi ambazo zimekwenda kwa Rais wa Bendi hiyo Chalz Baba. Mwanamuziki Kala Jeremiah yeye ametwaa tuzo tatu ambazo ni Msanii Bora wa Hip Hop, Wimbo Bora wa Mwaka na Mtunzi Bora wa Mahairi Hip Hop. Ommy  Dimpoz yeye ametwaa tuzo tatu ambazo ni Video Bora ya Wimbo ya Mwaka, Wimbo Bora wa Kushirikiana/Kushirikishwa na Wimbo Bora wa Bongo Pop Entertainment.

GPL

No comments:

Post a Comment