Friday, 14 June 2013

YAH: UTARATIBU MPYA WA KULIPIA ADA YA VISA YA KWENDA TANZANIA • Kwa wana-diaspora  wanaohitaji Visa ya Tanzania,
 • Tunapenda kuwaarifu kuwa kuanzia tarehe 1 Mei 2013, Ubalozi haupokei fedha taslimu wala “Credit Card” kwa malipo ya visa.
 •  
 • Malipo yote sasa yanafanyika kwenye akaunti yetu ya Benki ya NORDEA Plus Giro Na. 103 7471-8 kwa walipaji walioko Sweden. Wanaolipia nje ya Sweden watumie (BIC/Swift Address:NDEASESS na IBAN: SE2895000099604210374718 (bila kuacha nafasi).
 • Risiti ya malipo iambatanishwe na fomu ya maombi utakapotuma maombi kwa posta au utakapoleta maombi kwa mkono Ubalozini.
 • Tafadhali tunaomba ujiepushe na  usumbufu kwako   kwa kulipia ada ya visa Benki kabla ya kuleta maombi yako Ubalozini.
 • Taarifa hii ipo kwenye tovuti ya  Ubalozi tangu mapema mwezi Aprili kupitia “link” ifuatayo:http://www.tanemb.se//index.php?option=com_content&task=view&id=178&Itemid=36
 • Unakaribishwa pia kuwasiliana na Ubalozi kwa njia ya simu au barua pepe endapo utahitaji maelezo ya ziada.
 • Tunawaomba na tunawashauri muendelee kutembelea  mara kwa mara tovuti ya Ubalozi,www.tanemb.se ili kupata habari na taarifa mbali mbali kutoka Ubalozini.

 • Tunatanguliza shukrani zetu

 • Jacob Msekwa


KNY: BALOZI

No comments:

Post a Comment