Thursday, 8 August 2013

KANUNI KUMI ZA KUMJUA MAGANGA

1.Mkikutana mara ya kwanza anakusalimia saaaana.

2.Akiskia umepata kazi nzuri basi majungu yanaanza mara yule aaah amna bana kaajiriwa na waarabu tu.au yule hamna kitu ile kazi ya mjomba wake ye kamshikia tu kwa muda.

3.Ukimwambia nataka kuoa mkiwa mnalewa kitu cha kwanza anataka kumjua mwanamke wako nani,ukilogwa kumwambia habari ya kwanza itakua "aaah yule malaya achana naye,kwanza hujui ana ngoma?oooh shauri yako mwenzio juma na asumani walitafuna pale.(kichekesho ukimwonyesha kesho picha ya huyo mke unayetaka kumwoa atakwambia simjui kabisa huyu nani?

4.Akikuona mtu mwingine umevaa vizuri kumzidi yeye ananuna na kusema kijana anaanza kiburi huyu.

5.Ukila vizuri anaenda kwa mganga kumshtakia ikiwezekana kuloga kisa"huyu jirani yangu maganga kila siku anakula nyama wakati sie tunashindia mihogo.

6.Maganga anakua siku zote yuko ulaya lakini hajiamini tabia zake kila siku kama yuko kwao kijijini Nangulukulu kwenye kilabu cha chimpumu.

7.Maganga akinunua kiatu au suti mpya basi kila muda atakua anajiangalia kwenye kioo,treni,barabarani haamini kama hivyo vitu ni vyake kanunua.
**Maganga akimuona maganga mwenzie badala ya kujiskia vizuri na kusalimia ndo kwanza atatema mate pembeni kama kamuona gorilla.

8.Maganga siku zote anataka kufananisha miaka aliyokaa ulaya na mafanikio ya watu,siku zote hapendi kumuona kijana anakuja juzi na yeye kaja miaka hiyo naintiini kweusi lakini mita haisomi,we uje juzi halafu uko njema kwani una ukoo na kina Svensson. 

9.Maganga hachelewi kuandika barua uhamiaji akimuona maganga mwengine anazagaa zagaa mtaani akishtaki kwamba "kuna vijana hapa nawaona hawana makaratasi wanazurula tu kula kodi yetu."
utafikiri analipa hiyo kodi

10.Siku ya mwisho maganga anaweza kuchokwa hapa ulaya akiambiwa aende kwao Afrika umagangani hataki,hata wakodi greda haendi why!anaona sasa niende na zile nyodo alizotangaza kama yeye huku ni muheshimiwa,waziri wa mambo ya kimataifa na kushughulikia mambo makubwa makubwa serikalini leo arudi kule umagangania akiwa hana kitu mchovu kunuka(wengi wanakuwa hivyo)haiwezekani

mi kwetu ntarudi bana saa yoyote,mi sio Ericsson feki,homu kupo na ntarudi kwa hiyo we ukijiona una tabia moja kati ya hizo basi bila shaka we MAGAAAANGA TU!

mmh hii nime-copy tu mahala raia msiandamane

1 comment:

  1. Big upp Isaackin hapo kisu kimegonga mfupa. mimi ni maganga wa hapa Stockholm, hicho ulichokitupia hapo juu ni hali halisi iliyopo hapa sweden, na hapo umeigusa jamii yetu yote ya sisi kina maganga. Kiukweli wapo maganga walio positiv lkn ni wa chache ila maganga walio na negativity ni wengi sana mpaka wanakera.

    ReplyDelete