Thursday, 31 October 2013
KISEBEENGO BABA-MAQUISE ORIGINALE+VUMBI DEKULA
KWA UFUPI THIS WAS ONE OF MY FAVOURITE OLD SONG OF ALL TIME,NAKUMBUKA HII TUNE YA HAWA JAMAA ILIWAHI KUIGWA NA VIJANA JAZZ ENZI ZA HEMED MANETI.WALIWAHI KUPIGA NYIMBO WAKIIGA TUNE HII
PIA NISIKATAE KUSEMA KWELI ILIWAHI KUTOKEA NILIHUDHURIA ONYESHO LA MAQUISE DU ZAIRE MWAKA 88-89 PALE UKUMBI WA UTAMADUNI SINGIDA NA WALILETWA NA MBIO ZA MWENGE.THAT TIME NILIKUA SIRUHUSIWI KUINGIA UKUMBINI LAKINI NILIINGIA KIUJANJA TU NA NIKALA MUZIKI INAVYOTAKIWA.
MIZIKI HII ILIPIGWA NA TULICHEZA SAAANA,NA KIUKWELI MIAKA ILE KULIKUWA HAKUNA BENDI ILIKUA IMEKAMILIKA KAMA MAQUIS DU ZAIRE "WANA SENDEMA YA MOOOTO".NAKUMBUKA BALAA LA VUMBI KWENYE SOLO ILA SIWEZI KUMSAHAU NGUZA VIKING NAE AKIWA NDIO KINARA WA KULITWANGA SOLO KIUMARIDADI ENZI HIZO.
ANYWAY VUMDI DEKULA KAHANGA TUNAYE HAPA STOCKHOLM NA KESHO ANACHARAZA NYUZI BIN NYUZ KAMA KAWAIDA PALE SODRA.USIKOSE KUJA KUSIKIA VIBAO VIPYA NA VYA ZAMANI.
ISAACKIN ATAKUWEPO KUCHUKUA TASWIRA.
Dekula Band"Ngoma Ya Kilo"01-02/11/2013
"Wazee Wapewe" present's;
Lady Neema,Yaya Sella & Bobo Sukari.
Dekula Band"Ngoma Ya Kilo"
Place:Lilla Wien"Little Nairobi"
Date:01-02/11/2013
Time:21.00-01.00...
Addr:Swedenborgsg.20
Pendel:Södra station
Sunday, 20 October 2013
Ufoo Saro aelezea kilichotokea kabla na baada ya kupigwa risasi
MWANDISHI wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye hivi karibuni alikumbwa na madhila ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mzazi mwenzie, ameanza kufunguka kidogo kidogo na kueleza kwa kina jinsi tukio zima lilivyotokea.
Akizungumza kwa sauti ndogo na taratibu na gazeti hili kando ya kitanda alicholazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mwanahabari huyo alieleza kushangazwa na ujasiri na nguvu za aina yake ambazo zilimwezesha kutambaa na kujiburuza hadi eneo la karibu ya barabara ili kuomba msaada wa kukimbizwa hospitali.
Ufoo ambaye alionyesha dhahiri kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazozingira tukio lake, alisema tayari alikuwa amewahakikishia polisi waliofika kumjulia hali hospitalini hapo kwamba alikuwa akisubiri afya yake iimarike kabla hajaeleza kwa kina kila anachokijua kuhusiana na tukio hilo.
“Alifika hapa kunijulia hali na kuangalia maendeleo yangu afande Msangi na nikasema nitakuwa tayari kueleza kila ninachokijua baada ya afya yangu kuimarika. Nasikitika kuna watu wanasema mambo wakifikia hatua ya kutaka kuonekana wananifahamu vizuri kuliko hata ninavyojifahamu mwenyewe,” alisema akionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazoripotiwa kuhusu sakata lake.
Ufoo ambaye alifikishwa hospitalini hapo Jumapili ya wiki iliyopita kutokana na kujeruhiwa kwa risasi na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja alisema anamshukuru sana Mungu kwa uzima alionao sambamba na kuelezwa kupata faraja kubwa na kutiwa moyo na mwajiri wake, ndugu, jamaa na marafiki.
Mwanahabari huyo ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi mwilini mwake siku chache zilizopita, amelazwa katika chumba cha peke yake ambacho ingawa kina seti ya televisheni alisema alikuwa haruhusiwi kuiangalia kwa ushauri na maelekezo ya madaktari.
Huku akionekana wa chini ya uangalizi mwingine wa karibu na wa kudumu wa muuguzi ambaye muda wote wa mazungumzo haya alionekana kuwapo katika chumba hicho, Ufoo alisema alikuwa ana mapenzi makubwa kwa mzazi mwenzake huyo ambaye alipoteza maisha katika tukio hilo.
“Nilimpenda sana Antheri. Alikuwa kijana mtaratibu na mpole sana. Najua kile kilichotokea ni shetani tu na binafsi nilishasamehe alfajiri ile ile baada ya tukio lile,” alieleza Ufoo ambaye pia alimpoteza mama yake mzazi katika mkasa huo.
TUKIO ZIMA LILIVYOTOKEA
Ufoo ambaye mara kadhaa katika mazungumzo na gazeti hili alionekana kukunja uso akiashiria kupata maumivu, alionyesha eneo la chini ya bega katika mkono wake wa kulia lililofungwa na bandeji ambalo alisema ndipo alipopigwa risasi ya kwanza wakati akigeuka na kujaribu kuepuka mauti muda mfupi baada ya Antheri kumfyatulia risasi zilizomkuta mama yake mzazi.
Akijaribu kuvuta kumbukumbu ya tukio lilivyoanza, Ufoo alisema mzazi mwenzake huyo alifika nyumbani kwake akitokea Sudan alikokuwa akifanya kazi usiku huo huo wa tukio na akamtaka kwenda kwa mama yake (Ufoo) eneo la Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kabla ya kufika Kibamba na kwa sababu ambazo Ufoo hakuzieleza, alimkariri mzazi mwenzake huyo akisema alikuwa amefikia uamuzi wa kujiua yeye na mtoto wao.
“Hata sijui ni nini kilitokea. Wakati tukitoka nyumbani Antheri alianza kwa kuniambia kwamba alikuwa amepanga kujiua yeye na mtoto wetu,” alisema Ufoo kabla ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa na kuendelea na simulizi yake ya kusikitisha.
Akiwa na sura ya ujasiri, Ufoo anasema pamoja na kumwambia maneno hayo bado Mushi alimsisitiza kwamba waende kwa mama yake (Ufoo) baadae warudi kumchukua mtoto wao japo Ufoo hakusema walitaka kwenda wapi baada ya hapo.
Alisema walipofika nyumbani kwa mama yake walikwenda moja kwa moja sebuleni na wakiwa wamekaa kwenye makochi baada ya salamu za hapa na pale ghafla Mushi akasimama akamwambia mama yake Ufoo kwamba; “Mama nimeishafanya maamuzi”
Kwa mujibu wa maelezo ya Ufoo, baada ya Mushi kutamka maneno hayo ghafla akaingiza mkono nyuma ya suruali alikokuwa ameweka bastola yake na kisha akaichomoa.
Katika maelezo yake Ufoo alisema baada ya kuichomoa bastola hiyo mama yake naye alisimama na kwenda kujaribu kumpokonya, kitendo hicho kilimfanya amiminiwe risasi mfululizo.
Alisema kuona hivyo aliamua kukimbia kuelekea jikoni ambapo Mushi alimuona na kuanza kumiminia risasi ambayo moja ilimpata eneo la mkono wa kulia ambayo ilitokezea mbele na kuchana titi la kulia.
Kwa mujibu wa Ufoo jeraha hilo halikumfanya akate tamaa ya kunusuru maisha yake kwani alijaribu kukimbia ingawa Antheri alifyatua risasi nyingine kadhaa ambazo zilimpata juu kidogo ya mgongo na kutokea tumboni ambazo zilisababisha aanguke chini
Akiendelea kusimulia, anasema ingawa alikuwa akivuja damu nyingi, na huku akijiburuza ardhini, Ufoo alisema wakati akitambaa aligeuka nyuma na akamuona Antheri akijielekeza bastola eneo la kidevu na alipofyatua risasi alianguka chini.
“Nikiwa chini nilimuona Antheri akijipiga risasi kidevuni na akaanguka chini, sikujua kilichofuata baada ya hapo kwani niliendelea kujiburuza ili kuokoa maisha yangu,” alisema Ufoo
ALIVYOJIOKOA
“Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.
Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.
“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.
“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,” alisema Ufoo.
Alisema muda mfupi tu baadaye alitokea kijana aliyekuwa na pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda ambaye alimuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ya Tumbi na akakubali.
“Yule kijana aliniuliza iwapo nilikuwa ninao uwezo wa kujishikilia vizuri na niliposema nitaweza akanisaidia kupanda katika bodaboda.
“Wakati huo nilikuwa naona kama tumbo linazidi kujaa. Nikiwa kwenye pikipiki kuna wakati nilikuwa nikihisi kwamba naweza nikaishiwa nguvu na kuanguka katika barabara na kisha kupitiwa na gari na kupoteza maisha. Lakini nilipata ujasiri na kujishikilia,” alieleza kwa sauti ya chini.
Alisema anakumbuka wakati walipofika eneo la Kibaha ilipo mizani ya kupima uzito wa magari makubwa walikuta barabara ikiwa imejaa magari na yeye alimuomba dereva huyo wa bodaboda kupita hata nje ya barabara eneo la nyasi ili kumwahisha hospitalini jambo ambalo kijana yule alilifanya.
“Nilipofika eneo la mapokezi pale Tumbi nilimueleza muuguzi niliyemkuta kwamba nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi na nikamuomba asaidie kuokoa maisha yangu. Yule nesi alisita akitaka kwanza kupata kibali cha polisi (PF3) lakini nikaumuomba apigiwe simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Tumbi, Dk. Dattan ambaye tunafahamiana”
“Baada ya muda mfupi Dk. Dattan alifika na nikamweleza yaliyonipata na mara moja nikaanza kuhudumiwa kwa kuniwekea dripu, na nikamsikia akiwaeleza wauguzi kwamba isingekuwa busara kwa hali niliyonayo kama wangeanza kuchukua picha za X-ray kwani hatua hizo zingeweza kusababisha kupoteza maisha,” alieleza akikumbuka yaliyojiri hapo Tumbi.
Kwa mujibu wa Ufoo, akiwa bado ana fahamu alimsikia daktari aliyekuwa akimhudumia akiomba msaada wa gari la kubeba wagonjwa ili limchukue na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wito ambao ulijibiwa kwa maelezo kwamba lilikuwa halina mafuta.
Majibu hayo kwa mujibu wa Ufoo, yalisababisha daktari huyo aombe kuletewa gari la wagonjwa la wagonjwa maarufu (VIP) ambalo lililitwa na muda mfupi baadaye akapakizwa tayari kwa safari ya kukimbizwa Muhimbili.
Alisema wakati akikimbizwa Muhimbili anakumbuka namna alivyokuwa akipatwa na maumivu makali wakati wote gari ile ya wagonjwa ilipokuwa ikipanda matuta ya barabarani na kuna nyakati alikuwa akihisi kupoteza pumzi na kuishiwa nguvu.
MTANZANIA

R.I.P. Julius Nyaisanga"Uncle J"
BURIANI JULIUS NYAISANGAH.......UNCLE J
Nyaisanga( wakwanza kushoto) akiwa na wanamuziki wa Sikinde na MK Sound |
Jina la Julius Nyaisanga hakika litabaki kutajwa katika historia ya muziki Tanzania. Mtangazaji huyu ambaye alitokea Kenya na kuja kujiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam, alikuja na aina mpya ya utangazaji ambayo ilimfanya apate nafasi ya pekee katika nyoyo za wasikilizaji wa RTD kwa miaka yote aliyokuweko huko. Julius ambaye mwenyewe alisema alitengeneza staili yake ya utangazaji kwa kumuiga mtangazaji maarufu wa KBC Leonard Mambo Mbotela aliyejulikana sana kwa kipindi chake 'Je huu ni uungwana?' alikuja na utangazaji uliochangamsha sana kumsikiliza. Nyaisanga alikuwa Producer wa mamia ya nyimbo za bendi zilizorekodiwa na bendi mbalimbali katika studio za RTD miaka ya 80. Nilipata bahati ya kufanya nae kazi wakati nilienda kurekodi nikiwa katika bendi tatu tofauti, Orchestra Mambo Bado, Tancut Almasi Orchestra, na Vijana Jazz Band. Alishauri vizuri na matokeo yake ni nyimbo nyingi zilizopitia mikononi mwake zingali zinapendwa mpaka leo.
Pamoja na utangazaji, na u producer wa muziki, Nyaisanga alipenda muziki na wanamuziki, alikuwa rafiki wa wanamuziki wengi sana, alikuwa na tabia ya kutembelea bendi zinapopiga na aliweza hata kutembelea bendi nne au tano kwa usiku mmoja. Na hasa kama bendi iko katika ratiba ya kurekodiwa. Aliwahi hata kufika Iringa kutembelea tancut Almasi Orchestra kabla ya kurekodi toleo lao lililokuwa naule wimbo usiochosha Masafa Marefu. Nyaisanga alipita kwenye bendi kadhaa kututaarifu kuhusu kuanza kwa radio mpya ambayo ingekuwa katika masafa ya FM, na ndipo muda si mrefu Radio One ikaingia hewani wakati huo ikiwa pale katika jengo la NASACO ambalo lilikuja kuungua na baada ya kukarabatiwa sasa linaitwa Waterfront. Pia akiwa Radio One Nyaisanga aliendelea kuwa Nyaisanga, japo sera za Radio One hakika zilikuwa tofauti na zile za RTD, lakini pia huko mchango wake katika muziki ulikuwa mkubwa sana. Hatimae Nyaisanga alihamia Abood Radio Morogoro ambako amekuweko mpaka hatimae usiku wa kuamkia leo 20 October 2013, umauti umemkuta katika hospitali ya Mazimbu Morogoro kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na Kisukari.
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI UNCLE J
Source-kitime blog
Wednesday, 16 October 2013
Monday, 14 October 2013
Vumbi&Dekula band live 18-19/2013
Wazee Wapewe" present's;
Lady Neema,Yaya Sella & Bobo Sukari.
Dekula Band"Ngoma Ya Kilo"
Place:Lilla Wien"Little Nairobi"
Date:18-19/10/
Time:21.00-01.0
Addr:Swedenborg
Pendel:Södra station
season winter to hit smoother Stockholm
According to the latest forecast from the Swedish weather agency (SMHI) snow will hit Umeå in the north of the country along with Mora and Östersund in central Sweden on Thursday.
Residents living in the capital can expect sleet and possible wet snow on Friday as a result of chilly winds blowing down from the north of the country.
IN PICTURES: Stunning snaps from when snow first hit Stockholm last year
"No snow has fallen in Stockholm yet and this will be the first of the season," said meteorologist Lisa Frost to the Svenska Dagbladet (SvD) newspaper.
The snow is arriving about a month earlier than normal but weather experts said there is no correlation between an early snowfall and a particularly harsh winter.
It's unlikely that the snow will stick with temperatures returning to above zero after the early flakes, with the exception of Kiruna at the northern tip of the country.
"One should still keep in mind that there will be sleet passing by during Friday. For the first snow people aren't always properly prepared so you obviously need to be careful in out on the roads."
SEE ALSO: Read the weather forecast for your corner of Sweden
"It is not so much that the snow sticks but that in some localities there is a risk of slippery conditions," added Frost.
The weather is better down south with Malmö enjoying temperatures of 12C for most of the week with Gothenburg on the west coast just a degree lower.
Stockholmers will enjoy a peak of 12C early in the week before the mercury sinks to single digits ahead of the snow's arrival on Friday.
It's quite a contrast to last week's Indian summer's day when parts of the country were bathing in sunshine approaching 20C. Meteorologists said at the time that winter usually arrives properly between October 19th and November 1st.
The lokal
wadau mbalimbali walitembelea nyumba aliyowahi kuishi Mwalimu Nyerere akidai uhuru iliyopo Magomeni
Bango linalosomeka Nje ya Nyumba ya Kwanza aliyowahi kuishi Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda barabara ya ifunda 60
Hii ndio nyumba aliyoishi Hayati Baba Wa Taifa Mwl Julius Nyerere Kwa Kipindi Cha Miezi nane iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda, Barabara ya Ifunda namba 60 ambayo sasa imekuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Nyumba ya Mwl Nyerere
Baadhi ya Wakazi wa Jiji La Dar Wakiwasili kwenye Nyumba aliyokuwa anaishi Hayati Mwl Nyerere Kipindi hiko kwaajili ya kujifunza na kufahamu historia yake japo kwa kifupi
Wakazi wa Jiji la Dar Wakipata Maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wahudumu (hayupo pichani) wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda wakati walipofika leo kutembelea nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Hayati Baba wa taifa Mwl Julius Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa ifunda
Mmoja wa Kijana aliyefika kwaajili ya Kutembelea Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaani wa Ifunda Jijini Dar akiandika jina katika kitabu cha Wageni mapema leo wakati alipotembelea Nyumba Hiyo leo
Wakazi wa Jiji la Dar wakionyeshwa Chumba cha Watoto wa Kiume wa Hayati Baba Wa Taifa Mwl Juilus Nyerere na mmoja wa wahudumu wa Nyumba hiyo (hayupo pichani) wakati waliotembelea makumbusho ya kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere mapema leo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Jijini Dar
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akitoa maelezo ya Redio ya kwanza aliyopewa Mwl Nyerere kama zawadi na Malkia Elizabeth kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika kutembelea nyumba hiyo iliyotumiwa na Mwl Nyerere hapo Mhudumu wa nyumba hiyo akiwaonyesha wakazi wa jiji la Dar waliofika katika Nyumba hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akitoa maelezo kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika kutembelea nyumba hiyo iliyotumiwa na Mwl Nyerere hapo Mhudumu wa nyumba hiyo akiwaonyesha Rozari aliyokuwa akitumia Hayati baba wa Taifa Mwl julius Kambarage Nyerere
Mmiliki wa Lukaza Blog Josephat Lukaza pamoja na Wakazi wengine wakipata maelezo kutoka kwa Bi Theresia Gratta Makene (katikati) juu ya redio ya kwanza aliyopewa Mwl Nyerere Kama Zawadi kutoka Kwa Malkia Elizabeth
Wakazi wa Jiji la Dar wakiangalia baadhi ya Picha zilizobandikwa katika Kuta za Nyumba aliyokuwa akiishi Hayati Mwl Nyerere Kwa kipindi cha Miezi nane, Nyumba hiyo ipo Magomeni Mtaa wa Ifunda
Baadhi ya watoto waliofika Katika nyumba hiyo Kwaajili ya Kuona vitu mbalimbali alivyowahi kutumia Hayati Mwl Nyerere vilivyopo katika Nyumba hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda
Watoto waliofika mapema leo Katika Nyumba aliyowahi kuishi Hayati Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda wakiangalia vitabu vya Mwl Nyerere
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akielezea juu ya baadhi ya vyombo alivyowahi kutumia Hayati baba wa taifa Mwl Nyerere wakati akiishi katika nyumba hiyo iliyopo Magomeni mtaa wa Ifunda.
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Mwalimu Nyerere day tunaikumbuka kwa hotuba yake hii-rushwa
Baba wa taifa alikua km anaoteshwa,yale yote aliyozungumza na kusisitiza yasifanyike ndio yanayotokea sasa.rushwa nyumbani Tanzania imekua ni km halali yao.
kuanzia airport ukifika ni rushwa wanataka.njiani trafiki unao.ukiumwa ndio balaa.daktari bila chochote utaganda kwenye foleni siku nzima.hata ukiandikiwa dawa utauziwa feki,maans wachina nao wamehonga wameingiza madawa feki.ole wako ufanye makosa sasa ukutane na polisi au mahakama.huko ni kwamba wanaomba rushwa km wanakudai.maana watakwambia toa laki 2 tumalize kesi,ole wako utoe watakwambia haitoshi ongeza 50,000.ukiongeza na wao ndio wanaongeza.mwisho unajikuta umeliwa laki 5 kimasomaso.
hii imenitokea mi mwenyewe na mpk sasa sijui nchi inaelekea wapi.
Happy Birthday mdau Lomunyaki Letara
Mdau wetu huyu amefikisha miaka kadhaa ya kuzaliwa na blog hii inamtakia kila la kheri na maisha marefu
Happy birthday Lomu
Happy birthday Lomu
Sunday, 13 October 2013
Ufoo Saro afanyiwa upasuaji baada ya kupigwa risasi na aliyekua mchumba wake ambaye amejiua pia kwa risasi
Baadhi ya waandishi na wananchi wakiwa wamekusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujua hali ya Ufoo.
Mtangazaji wa ITV na Radio One, Ufoo Saro amefanyiwa upasuaji baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi na mzazi mwenziye aitwaye Anther Mushi mapema leo. Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Ufoo alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi Annastazia Saro baada ya kutokea mgogoro baina yake na mzazi mwenziye. Katika tukio hilo, Anther alimpiga risasi na kumuua mama Ufoo kisha na yeye akajilipua kwa risasi baada ya kumpiga risasi Ufoo. Kwa sasa Ufoo amehamishiwa katika wodi ya Kibasila anapoendelea kupatiwa matibabu. Umati wa watu ulikusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi ili kujua hali ya mtangazaji huyo. Kwa habari zaidi kuhusu tukio hili soma gazeti la Uwazi Jumanne.
(PICHA ZOTE NA MAKONGORO OGING / GPL)
Friday, 11 October 2013
Ukweli kuhusu Wema na Diamond huu hapa
Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond na Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond, ‘Temptations’ haipo na kama unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.
Diamond na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.
Wema, Diamond na binamu yake Rommy wakiwa Hong Kong |
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air Asia.
“Nilipanda na Diamond flight moja from KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote ndo alikua akiyafuata hongera zao,” alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na yeye ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Penny |
Hivi karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.
“Not the easiest relationship I’ve ever had..but its the most intresting! When I’m down, he would make me feel on top of the world, my bestfriend, my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a blessing to have met you, u taught me that love is just Me&You the rest shouldnt matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless u a million more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable mind, through the ups and downs Im gona hold you down til God says so..you have taught me that love conquers all, that Love is pain, but the pain is worth the while..I love you baby,” aliandika Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia jarida la Mzuka kwenye makala ambayo haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama nina uadui naye personally, sijui yeye na urafiki hatuna. Let me just say kwamba sio kwasababu ya Diamond. Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna issue zetu nyuma ambazo hazikuwa resolved so tulikuwa tuna distance mimi na yeye. Tulikuwa hatuongei maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane, we had our own issues kwahiyo hatukuwa marafiki vile tena kama tulivyokuwa zamani. So mimi kuwa na uadui naye sidhani kama nina uadui. Mimi am happy unajua, mimi ndo hivyo mimi naishi maisha yangu am happy na nilichonacho am happy with my man, am happy na watu wangu so am good mimi sina tatizo naye kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.
“It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond waliwahi kuingia kwenye ‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada ya Diamond kumrekodi mpenzi wake huyo wa zamani alipompigia na kuisambaza sauti kwenye vyombo vya habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.
Updates ni kwamba Penny hakuzimia wala hakulazwa na anaendelea na maisha yake.
Thursday, 10 October 2013
WEMA NA DIAMOND NDANI YA MALAYSIA
Hii ndio mambo ya mapenzi,waliosema ndugu wakipigana shika jembe ukalime hawakukosea,sasa inakuja wapenzi wakigombana we inabidi tu utupe jembe kabisa na kuanza kuimba wimbo wa Gurumo "ukiona mtu mzima analia"ujue kuna jambo.maana kijana wetu maarufu huyu siku ya kuanza kulia machozi tena ikiwezekana ya damu tutasikia tu.kwa maana haya mambo ya kuatanga na njia huku na kule hayana mpango,inabidi sometyme atuulize sie baba zake wadogo.
kwa analysis ya haraka haraka kwa watakaoelewa kuna maswali ya msingi.
*je Wema anamhitaji tena huyu jamaa au anataka kumuharibia tu maisha yake?
*kama walikutana hiyo ni ishu iliwahusu wao na makubaliano yalikuwa siri iweje leo imevuja kila mahali.
*Wema ana mshua wake anayemuweka mjini,ina maana ana uwezo wa kusafiri,kukodi hotel na kutumia fweza kiasi chochote akitaka kwa sababu kuna pimbi mmoja atarudisha pesa.
*Diamond kuwa na Wema tena si kitu cha kushangaa sababu kidume yeyote Ex wako akileta pirog yake na bado analipa unakanyaga twende maswali kesho.
mambo haya ni rahisi kujibu inabidi dogo awe mbishi tu.lakini asishangae sana maana huu ni wakati wake na unapita kama upepo,kuna mtu aliitwa Mr Nice mzee wa kidali po!.aliwasha moto sana hata hapa Sverige.kwa sasa jamaa anauza bia pale urafiki club Manzese.
mpaka hapo ndio naelewa wasanii safari yenu ya kula bata si ndefu kihivyo inabidi mjipange.
kuna list hii ya wasanii waliwahi kula bata:
MR NICE
Inspecta Haroun
Juma Nature
Ferouz
T.I.D.
Daz Baba
Ray C
Sister P
na wengine kibao
Saturday, 5 October 2013
Friday, 4 October 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)
Championi Jumatano lilimshuhudia kiungo huyo aliyewahi pia kuichezea Panellenois ya nchini Sweden, akiichezea timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Manzese dhidi ya Villa Squad ya Magomeni, mechi ilipigwa kwenye Uwanja wa Karume uliopo Ilala ambapo Friends ilishinda 2-1.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Credo alisema kuwa kwa sasa amesaini kuichezea timu yake hiyo ya awali kutokana na kusubiri kukamilika kwa mipango yake ya kwenda kukipiga kwenye klabu moja iliyopo nchini Sweden.
Alisema kuwa anashindwa kabisa kukaa bila kucheza mpira wa ushindani, ndiyo maana akajiunga na timu hiyo kwa sasa ambayo hajasaini kuitumikia kwa miaka bali ni fomu inayomuonyesha kuwa kwa sasa anamilikiwa na timu fulani.
“Nimerudi kwenye timu yangu ya nyumbani kwa muda nikisubiri mipango yangu ya kurudi Sweden ikamilike, kuna hatua nzuri, kwa hiyo mipango itakapokamilika muda wowote nitaondoka.
“Naweza kuondoka muda wowote kama nikipata timu nje ya nchi lakini kama nikipata Tanzania lazima Friends izungumze na hiyo timu kutokana na fomu niliyosaini ambayo inanionyesha kuwa ninamilikiwa na Friends kwa sasa msimu wote huu,” alisema mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea JKT Ruvu.