Monday, 14 October 2013

Mwalimu Nyerere day tunaikumbuka kwa hotuba yake hii-rushwa


Baba wa taifa alikua km anaoteshwa,yale yote aliyozungumza na kusisitiza yasifanyike ndio yanayotokea sasa.rushwa nyumbani Tanzania imekua ni km halali yao.
kuanzia airport ukifika ni rushwa wanataka.njiani trafiki unao.ukiumwa ndio balaa.daktari bila chochote utaganda kwenye foleni siku nzima.hata ukiandikiwa dawa utauziwa feki,maans wachina nao wamehonga wameingiza madawa feki.ole wako ufanye makosa sasa ukutane na polisi au mahakama.huko ni kwamba wanaomba rushwa km wanakudai.maana watakwambia toa laki 2 tumalize kesi,ole wako utoe watakwambia haitoshi ongeza 50,000.ukiongeza na wao ndio wanaongeza.mwisho unajikuta umeliwa laki 5 kimasomaso.

hii imenitokea mi mwenyewe na mpk sasa sijui nchi inaelekea wapi.

No comments:

Post a Comment