Thursday, 18 April 2013

UNAIKUMBUKA WALAY DANIKO-JB MPIANA IPATE HAPA LIVEkipindi bolingo ikipigwa sawa sawa.JB Mpiana alifika hapa stockholm mara ya mwisho mwaka 2007.hata hivyo siku hiyo perfomance yake ilipooza kwani ndio ilikua kipindi akiugulia machungu ya kuporwa mke na Didi kinuani.toka hapo kwa sasa sioni wanamuziki kuja sana Europe kwani kuna hawa jamaa wakimbizi wa Kicongo wanajiita Le-combantant wanaandamana kupinga concert kufanywa ulaya wakidai kwamba nchi yao ina matatizo hawahitaji starehe(kama kweli vile).mfano mdogo ni pale alikuja Fally Ipupa mara ya kwanza wakatishia wametega bomu ukumbini.waswede kama kawaida yao wakasema ok then hamna concert.mara ya pili pia kwa huyo huyo Fally waliandamana pale Gamla stan nje tu ya ukumbi ambao Fally ipupa alikua akipiga,baada ya hapo waliingia watu ishirini tu kwani wale waandamanaji walikua nje wakizuia watu hata waliolipia ticket kabla kuingia!
hao jamaa wana mtandao mkubwa,wapo Belgium,Canada,na nchi zingine kibao.

unaweza kuwaona hapo chini walipoandamana kupinga concert ya Fally Ipupa.Maganga wana kaaaaz kwel kwel!

No comments:

Post a Comment