Sunday, 15 September 2013

Picha zaidi za padre aliyemwagiwa tindikali Zanzibar


Padre Ancelmo Mwang'amba anavyoonekana pichani baada ya kumwagiwa tindikali.
Padre Ancelmo Mwang'amba akiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar anapopatiwa matibaabu.
Padre Ancelmo Mwang'amba wa Kanisa Katoliki alimwagiwa tindikali jana akiwa anatoka nje ya duka linalotoa huduma ya mtandao 'Internet Cafe' maeneo ya Mlandege Zanzibar. Padre Ancelmo ambaye anafanya kazi zake katika Kituo cha Malezi cha vijana cha Cheju kinachoendeshwa na Kanisa Katoliki kisiwani Zanzimbar, alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana ambao walitokomea kusikojulikana baada ya kutenda unyama huo. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii vimearifu kuwa, tindikali hiyo imemuathiri Padre Ancelmo hasa sehemu za usoni na kifuani. Kwa sasa yupo hospitali kuu ya Mnazimmoja Zanzibar akiendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment