Friday 30 September 2011

Makamu Wa Rais Akutana Na Waziri Wa Maendeleo Na Ushirikiano Wa Kimataifa Wa Sweden





1. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo jijini Stockholm Sweden hivi karibuni.   



2. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha yenye Taswara ya mjini wa Zanzibar, Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati Makamu alipofika Ofisini kwa waziri huyo jijini Stockholm Sweden kwa mazungumzo hivi karibuni. 


3. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akichangia katika kongamano la lililoandaliwa na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, kuhusu nafasi ya uhusiano wa Tanzania na Sweden, lililofanyika jijini Stockholm Sweden majuzi


Picha na Muhidin Sufiani-OMR


No comments:

Post a Comment