Thursday 22 September 2011

MAMA MKENYA AKAMATWA KWA KUTUHUMIWA KUWAUA WANAE WAWILI SWEDEN










 

mkenya mama wa watoto wawili anashikiliwa na polis stockholm kwa tuhuma za mauaji ya wanae wawili.yasemekana watoto hao walipotea toka jumapili jioni na hivyo kuanza kutafutwa baada ya tukio la kutoonekana kuripotiwa polisi na baba mtu
baada ya kuripoti polisi na polis kuanza msako ndipo jumatatu mchana walipowakuta watoto hao ndani ya maji ziwani wakiwa wamekufa na wakiwa na majeraha.
inasikitisha kuonekana asilimia kubwa ya waafrika wanapata msongo wa akili na mawazo wakiwa nje kiasi cha kufikia kujikatili wao ama kukatili maisha ya wengine.tatizo liko wapi?
maana nashindwa kuelewa,kabla mtu hujasafiri kwenda ulaya unakuwa na ndoto nyinginyingi nzuri nzuri za maisha matamu utakayopata huko ulaya lakini inakua shubiri mara unapofika huko na kukutana na kila aina ya udhalilishwaji na kuwekwa grade la chini.yeah huwa tunajitutumia ili na sisi tuonekana wa ulaya ikiwezekana hata kuweka blonde color kwenye nywele tunaweka na kuongea kiswidi ama kikabila chao lakini wapi wee kama ni ngozi na ni maganga basi itabakia kuwa hivyo.wengine tunatembea mitaani huko tukiangalia maghorofa waliyojenga wenzetu wenye nchi gamla stan ama sodelmalm tunatembea vifua mbele huku tukijiita MI MSWIDI.
hiyo ni kuiongopea nafsi yako tu maana kwenu ni kwenu mi najivunia kutoka kwetu huko iponjola tukuyu,kuhusu hiyo mtu haniambii kitu,hii mambo ya kungangana na nchi za watu sio kabisa
tukirudi kwenye pointi nashindwa kuelewa huyu mdada imekuwaje kafikia kufanya hatua kama hiyo.ni mdada  namjua na mni muhudhuriaji mzuri wa kanisa na mwimbaji saaana wa injili sasa imekuwaje?
kingine ni kwamba nasikia mwadada huyu alikuwa kapagawa na maisha ya stockholm yanamchanganya na pia nyumbani huko nairobiya pia haikuwa inaenda vizuri,lakini ndio ufikie kuua watoto wako?
kama vipi si ujiue mwenyewe sasa,au ukishindwa kabisa theres always second chance si angerudi huko kwao kenya akagombee hata u katibu kata au uenyekiti wa kijiji.
kwanini inakuwa ngumu sana kurudi makwetu jamani,tukishalowea huko wenzetu wameweka miundo mbinu mizuri ni kwa ajili yao sio yetu sisi wakimbizi,sisis tunapewa favour tu.inabidi tukazane kujenga kwetu ili japo pafanane.tutaishia kuwa wakimbizi wa nchi za watu mpaka lini?wenyewe hawatutaki invandrare lakini sie tumekomaa tu mi mswidi mi mswidi na wenyewe wanatufukuza toooka.na sie tunakataa nej mi mswidi.
jamani tusijishushe kihivyo maisha yakitubana huko tuwe huru kurudi makwetu,japo utakuta nduguzo bado wanakusubiri kwa upendo wa dhati,utakuta pia vibaka wanakusubiri kwa hamu mugawane ulichochuma,pia usisahau polis wanakusubiri utaanza nao toka airport mpaka mabarabarani lazima uwagawie ulichochuma,hiyo ndio burdani ya homu.licha ya yote hayo bado home is sweet,ni kwenu tu.kwahiyo wandugu ni wito kama maisha yanabana huko ulaya rudini nyumbani huku japo mgombee ujumbe wa chadema maisha yataendelea kuliko mnyanyaswe mpaka kufikia kujitoa uhai.
haya mi naishia hapo kabla umeme haujakatika

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA na HAPA



1 comment: