Saturday 24 September 2011

MISS KINONDONI ATOWEKA KWAO



Mshiriki Miss Tanzania 2011, Husna Maulid (pichani) anadaiwa kutoweka nyumbani kwao na hajulikani alipo.
Husna, aliye Miss Kinondoni namba mbili mwaka huu, anadaiwa kurejea nyumbani kwao Magomeni Kagera, Dar baada ya shindano la Miss Tanzania 2011 na kukaa siku tatu kabla ya kutoweka.
Hawa ambaye ni mama mdogo wa Husna, aliliambia Risasi Jumamosi ‘The 5star Paper’ kuwa awali alipoondoka, walidhani angerejea lakini siku zinaendelea kukatika bila kuonekana.
Mama huyo, alilitupia lawama Shindano la Miss Tanzania kwamba ndiyo chanzo cha mmomonyoko wa tabia kwa mrembo huyo.
“Yaani Husna toka ashiriki mambo ya u-miss kawa mtu wa ajabu, hata hizo siku tatu alizorudi nyumbani alikuwa mtu wa kuzurura na teksi tu, kwa sasa anaposhinda na kulala anapajua mwenyewe,” alisema Hawa na kuongeza:
“Tunahangaika kumtafuta angalau tujue alipo lakini tunajua yule ni mtu mzima, mjini hapa ni mwenyeji, kwa hiyo atakuwa sehemu anayoijua mwenyewe.”
Gazeti hili, lilifanya jitihada za kumtafuta Husna lakini halikufanikiwa na simu ya mrembo huyo, muda wote ilikuwa haipatikani.
Fainali za Miss Tanzania 2011, zilifanyika Septemba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Tangu kufanyika kwa shindano hilo, leo ni siku ya 14, ukitoa zile tatu ambazo alifika nyumbani kwao, ina maana Husna hajulikani alipo kwa siku 11 sasa.
Kabla ya kung’ara kwenye mashindano ya u-miss, akianzia kitongoji cha Sinza, Husna alishatia fora kwa kupiga picha chafu tofauti ambazo zilimuonesha akishiriki vitendo vya ngono na wanaume wawili tofauti

SOURCE:GPL

No comments:

Post a Comment