Saturday 17 September 2011

TBS kukagua simu za Kichina



 Send to a friend

Ibrahim Yamola na Zuberi Salum
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesema litaanza kuzifanyia vipimo simu za mikononi, ili kubaini ubora wake.

Hatua hiyo inakuja baada ya TBS kulalamikiwa na baadhi ya watumiaji wa simu kuwa simu zao hazina viwango, kutokana na mwingiliano wa mawimbi ya umeme na hata kusababisha hitilafu katika kompyuta.Mkazi mmoja wa Tabata Dar es Salaam, Gabriel John aliiambia Mwananchi kuwa kompyuta yake ndogo  ilizimika gafla baada ya simu ya mkononi kuita na kwamba hadi  sasa haijapona

“Hii inamaanisha kuwa hizi simu za kichina hazina viwango kwa sababu zinaingiliana sana na  mawimbi ya umeme,”alisema.Jana katika Maonyesho ya Mtandao wa Maendeleo wa Wanawake Wajasiriamali (TWENDE), Ofisa Masoko wa TBS, Daudi Mbag, aliliambia Mwananchi kuwa, wamejipanga kutatua tatizo hilo linalolalamikiwa na watumiaji wengi wa simu.

“Mchakato wa kuzifanyia vipimo simu za kichina ili kujua kama ziko katika viwango vinavyokubalika, umechelewa kuanza  kwa sababu ya kukosekana kwa vifaa vya chunguzi lakini kwa sasa tuko katika hatua za mwisho na hivi punde zoezi litaanza” alisema Mbanga

Maonyesho hayo yanayofikia kilele chake kesho katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, yalizinduliwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba ambaye aliwaasa wajasrliamali kujiunga katika vikundi vinavyotambulika ili Serikali ianza kuwapa mikopo

“Pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali katika kuleta usawa wa kijinsia, bado hali ya wanawake nchini kiuchumi si ya kuridhisha, hivyo nawaombeni mjiunge katika vikundi na kuanzisha Saccos ili Serikali iweze kuwasaidia kwa pamoja.

mwananchi

No comments:

Post a Comment