Friday 16 September 2011

MNIGERIA ALIYETOKA SIMBA ATAMBA SWEDEN





MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Emeh Izuchukwu anaishi kama mfalme kutokana na kuonekana ni lulu katika timu yake mpya ya Assyriska FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden.

Izuchukwu raia wa Nigeria amekuwa lulu kutokana na kupachika mabao saba katika mechi sita alizocheza, hali inayomfanya aonekane ni tegemeo.

Akizungumza kutoka Sweden, Izuchukwu alisema baada ya kutua nchini humo, mambo hayakwenda vizuri.

“Kuona hivyo niliamua kujituma na kufanya mazoezi mara tatu kwa siku. Nilijua Norway mambo pia



 hayakuwa mazuri, sikuona sababu ya kukata tamaa hapa Sweden, umri wangu unaruhusu.
“Nilianzia kwenye timu ndogo, lakini sasa nitapiga hatua tu. Ninaamini baada ya muda nitaondoka hapa na kwenda kwingine,” alisema.

Joel Thomas, Mtanzania anayeishi nchini humo alisema Izuchukwu amekuwa nyota na ni vigumu kuamini alikuwa anachezea Simba.

“Wengi wanaamini ni mchezaji kutoka hapa hapa Ulaya, nimeshangazwa sana kusikia ametokea Simba. Hapa ni staa mkubwa kwa kipindi hiki.”

Izuchukwu aling’ara Simba akiwa na Mnigeria mwingine, Orji Obina. Baadaye aliondoka nchini baada ya kuuzwa katika klabu ya Kongsvinger ya Norway lakini huko akashindwa kuonyesha cheche zake kabla ya kuhamia Sweden.



GPL

No comments:

Post a Comment