Tuesday 20 September 2011

TANGAZO LA MKUTANO WA MAKAMU WA RAIS, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL NA WATANZANIA WAISHIO NCHI ZA SKANDINAVIA



            Makamu wa Rais wa Tanzania, 
Dkt. Mohammed Gharib Bilal atatembelea Uppsala             

Sweden kwa ziara ya kikazi.
       Wakati wa ziara hii Mheshimiwa Bilal atapenda kukutana  na Watanzania waishio nchi za Scandinavia siku ya Jumapili tarehe 25 September 2011 kuanzia saa tisa na nusu alasiri katika ukumbi wa Hoteli ya Clarion Gillet uliopo kwenye anwani ifuatayo:


Dragarbrunnsgatan 23, 75320, UPPSALA, SWEDEN.

Watanzania mnaombwa mjitokeze kwa wingi ili mpate fursa ya kufahamiana na kujumuika na Mheshimiwa Makamu wa Rais kwenye mkutano huu.

Tafadhali mnaombwa sana kuzingatia muda.

No comments:

Post a Comment