Monday 3 October 2011

AUNAFUNGIWA KUUZA FILAMU SABABU YA UCHOYO WA KUTOA URODA




Wewe ni shabiki wa kazi za Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’? Umeweka utaratibu wa kila mwezi kwenda maktaba kununua filamu mpya ya staa huyo? Itabidi usubiri sana, sistaduu huyo amewekwa kifungoni kwa mwaka mzima, hatakiwi kucheza filamu yoyote.Sababu ni nini? Inadaiwa ni kisa kizito. Inaelezwa kuwa mabarazameni ambao ndiyo ‘ma-tuff wallet’ kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Kanumba ndiyo waliopanga kumpoteza duu huyo.Aunt amepigwa chini kwenye Klabu ya Wasanii wa Filamu, Bongo Movie Club. Jina lake limepelekwa kwa kampuni moja inayoongoza kwa kusambaza filamu za Kibongo na imetakiwa isithubutu kuingiza sokoni kazi yoyote ambayo Gwantwa anaonekana ndani.

Kisa kizito ni mapenzi. Inabainishwa kuwa Aunt ni mchoyo wa penzi lake, kwamba kuna mwekezaji mmoja kwenye kiwanda cha filamu ambaye amefukuzia penzi lake muda mrefu bila mafanikio, hivyo ameona bora ambanie. Kama mbwai mbwai!
Inaelezwa kuwa hasira za mwekezaji huyo, zilisababisha Ray na Kanumba waketi kabla ya kuamua kumuondoa Aunt kwenye ulingo wa maigizo ya filamu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Wanaharakati wa Kijinsia (TGNP) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), wanaweza kuchukua ‘tipu’ hii na kuifanyia kazi kwa ajili ya staa huyo ambaye jina lake linakita vilivyo kwenye tasnia ya maigizo.

USHASIKIA FUMANIZI?
Hapa juzikati, ulienea uvumi kwamba Aunt akiwa na Kanumba wakifanya mambo yao, walifumaniwa na mshkaji anayemmiliki mrembo huyo aliyedaka krauni ya Miss Mwanza 2006 kabla ya kutusua Miss Kanda ya Ziwa na kushiriki Miss Tanzania.

Kutokana na wingi wa SMS kuelezea fumanizi hilo, gazeti hili lilimuuliza Kanumba ambaye alikana kufumaniwa na Aunt, zaidi hakutaka kuzungumza chochote, wakati mrembo huyo yeye alisema kuwa fumanizi ni ‘famba’ na kwamba kuna stori zaidi ya hilo fumanizi, ingawa aligoma kuisema.

Showbiz ilifanya uchunguzi na kubaini madai kuwa siku ya tukio, kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar, mwekezaji wa kiwanda cha filamu anayemtaka Aunt kwa muda mrefu, alilazimisha kuondoka na mrembo huyo ili wakaduu lakini binti aligoma.

“Aunt alichomoa kwenda na huyo jamaa, kwanza alikuwa na mtu wake, pili hakuona sawa kulazimishwa kufanya mapenzi na mtu asiyempenda,” sosi wa Showbiz alisema na kuongeza: “Huyo jamaa baada ya kuona anakataliwa na ameshafukuzia muda mrefu, aliamua kumzaba makofi Aunt.

“Unajua tena kofi la mwanaume kwa mwanamke, Aunt alianguka chini kama mzigo, jamaa wa Aunt (jina tunalo) alipoona mpenzi wake amepokea kipondo, ilibidi ainuke mbio kwenda kuzipiga, ikatokea bonge la mtafaruku. Pale Leaders kulikuwa na wasanii wengi wa filamu ambao ‘walimgadi’ yule mwekezaji wa filamu.
“Wasanii wakampa kipondo yule mpenzi wa Aunt. Walikuwa wasanii wengi, sasa watu walioshuhudia vurugu, wakadhani Aunt alikuwa na Kanumba ndiyo wakafumaniwa lakini ukweli lile halikuwa fumanizi.

“Matokeo ya ugomvi ikaonekana ni lazima Aunt akomeshwe. Ray na Kanumba walikomalia bifu hilo kwa kumfungia kucheza filamu kwenye makampuni yao, baadaye ushawishi ukaenezwa. Akafungiwa Bongo Movie na msambazaji mkuu naye ameshaambiwa asipokee filamu zake.”

UNYANYASAJI WA KINGONO NI MWINGI
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba aliiambia Showbiz kuwa hajaambiwa na Aunt kuhusu kufungiwa au manyanyaso anayopata lakini anafahamu kwamba manyanyaso ya kingono kwa wasanii wa kike ni mengi.

“Najua msanii wa kike hana haki, anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi na mtu, akikataa basi atafungiwa asionekane kabisa kwenye filamu,” alisema Mwakifamba. “Tatizo ni kubwa kwa sababu kuna watu wana ushawishi mkubwa mpaka kwa wasambazaji.
“Msambazaji akiambiwa asichukue filamu ambayo imechezwa na msanii ambaye hatakiwi, yule msanii anaweza kupotea jumla kwa sababu binafsi. Hayo ndiyo mambo tunayopaswa kuyachukulia hatua.”

Mwakifwamba aliongeza: “Kampuni inaweza kukataa kufanya kazi na Aunt lakini mamlaka ya kumfungia yapo kwetu shirikisho. Msanii hawezi kufungiwa kienyeji, lazima kuwepo na barua ya onyo, akirudia ndiyo anafungiwa baada ya vikao halali kumjadili na mhusika kuitwa na kujieleza.
“Utaratibu wa kumfungia mtu kienyeji haupo na siyo haki kwa mujibu wa sheria.”

AUNT MUOGA
Staa huyo alipoulizwa na Showbiz kuhusiana na sakata hilo, alijibu: “Jamani hayo mambo sitaki kuyazungumzia. Sihitaji migogoro iongezeke.”

KANUMBA AUFYATA
Kanumba ndiye msemaji wa Bongo Movie Club lakini kwenye hilo aliufyata kuzungumza: “Mwenyekiti ndiye aongelee hilo, mimi hapana, kwanza nipo bize sana, narekodi.”

JB KASIMAMIA WAPI?
JB alipoulizwa na Showbiz alisema: “Aunt hajafungiwa, nazungumza kama mwenyekiti. Kwanza sitaki hili jambo lienee kwenye magazeti.”
Punde, JB alikengeuka: “Iwe Aunt amefungiwa au hajafungiwa, sitaki kutoa ushirikiano. Mambo yetu tunataka tufanye bila kuingiliwa na magazeti.”

RAY NAYE MMH!
Ray alipoulizwa na Showbiz alijibu: “Hakuna kitu kama hicho, Aunt hajafungiwa lakini ongea na msemaji wa klabu (Kanumba).”

SAKATA LINAENDELEA
 JB, Kanumba na Ray pamoja na menejimenti ya kampuni hiyo ya usambazaji lazima wazungumze kwa uwazi na kuachana na mambo ya kandokando. Kumfungia kucheza filamu staa mkubwa kama Aunt bila vikao, onyo wala barua ya kujieleza si jambo dogo. Tunazidi kufuatilia na kuandika.



chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment