Thursday 27 October 2011

WEMA,WOLPER NA DIAMOND TENA




 MADUU wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe, wapo kwenye vita nzito, chanzo kikiwa ni penzi la mwana Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Wema na Wolper kwa sasa ni afadhali ya paka na panya, wanapakana mbovu, ‘wanavuana nguo’ mbele ya jamii na kila mmoja ‘amemtangazia njaa’ mwenzake.

Amani linamiliki data za uhakika kuwa kutokana na ‘bifu’ la mastaa hao, tayari makundi mawili yameshaibuka, moja likimpa kampani Wema, lingine lipo ‘beneti’ na Wolper.

Upande wa Wema, mashosti wake wakubwa ni Kajala Masanja na Elizabeth Michael ‘Lulu’, wakati kwa Wolper, shoga yake mkubwa ni Christine Manongi ‘Sintah’.

Sistaduu anayevutia zaidi kwenye muvi, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ inadaiwa yupo kotekote na anapigwa dongo kwamba ni msaliti (snitch).

AMANI LIMEJUAJE?
Ijumaa iliyopita (Oktoba 21, mwaka huu), gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo namba 745, liliandika habari ya Wema na Diamond kumwagana.

Baada ya Wolper kunasa habari hiyo, alichukua kipande cha gazeti hilo na kukitundika kwenye safu yake ya mtandao wa ujumbe wa simu aina ya Blackberry (Blackberry Messenger, BBM).
Pamoja na kipande hicho cha gazeti, Wolper aliandika: “Yamekwisha.”

Wolper anadaiwa kuendelea kuchombeza maneno: “Kuachwa kubaya.”
Baadaye Wema alijibu mapigo kupitia anuani yake ya BBM kwa kuandika: “True love never die (penzi la kweli halifi).”
Wema aliendelea kushusha madongo: “Mimi na Diamond tunapendana, ananipenda sana, hatuwezi kuachana. Wewe ndiyo unakimbiwa na wanaume.”

Kwa upande mwingine, Wolper baada ya habari kwamba Wema na Diamond wametosana, alimuandikia SMS ‘bwa mdogo’ huyo anayebamba ‘kitaa’ kwa ‘songi’ lake la Moyo Wangu. Ujumbe ulisomeka: “Hi baby.”
Diamond alijibu: “Usiniite baby, mke wangu hapendi.”

Baada ya hapo, mazungumzo kati ya mwana Bongo Fleva huyo na Wolper yaliendelea hivi;
Wolper: Kama mkeo hapendi, mimi nina nafasi yangu na yeye anayo ya kwake.
Diamond: Wewe una nafasi gani kwangu?

Wolper: Unajua mwenyewe nafasi yangu kwako.
Inadaiwa kuwa Diamond alimuonesha Wema SMS za Wolper, hivyo kuzidi kumtibua.

BBM TENA!
Baada ya Wema kuona Wolper anamsakama, alirejesha mashambulizi yake kwa njia ya BBM.
Kwa kuanzia, Wema aliponda picha za Wolper alizopiga akiwa amenyoa nywele na kuweka rangi nyeupe mithili ya Amber Rose.

Katika picha hizo, Wolper aliandika Amber Rose bila kuongeza neno lolote.
Wema alimponda Wolper kwa kuandika kwamba si Amber Rose kisha aliponda: “Amber Rose Bongo?”
Wolper alijibu mapigo, akachukua picha ya Wema (mbaya), akaiweka mtandaoni, kisha akaandika: “Basi huyu ndiye Amber Rose. Ila nimeipenda sana hii picha.”

Kwa shambulio hilo, Wema alikuja juu na kumchana Wolper kuwa hana ujanja wowote kwa sababu ni mgeni mjini na kwamba tangu ameingia Dar, hana hata Krismasi tatu.
Wolper naye akamvua Wema kuwa ni supastaa ambaye hana hata kitanda kisha akapiga picha pea za viatu vyake na kuahidi kuviuza ili amnunulie ‘cha kulalia’.

MAKUNDI
Kutokana na bifu hilo, Kajala na Lulu wamekuwa wakimsapoti Wema kumchakaza Wolper kwa kuandika au kuchangia ujumbe wenye sura ya kumchana.

Amani lilipozungumza na Kajala kuhusu hilo, alisema Wolper ni mchokozi kwa sababu anaingilia uhusiano wa Wema na Diamond.

Aliendelea: “Asili ya Wolper ni mchokozi. Namsaka, nikimkamata atanitambua.”
Wolper alipoulizwa alijibu: “Mimi sijui chochote, nakumbuka picha zangu ndiyo watu walichangia wakiniita Amber Rose.”

Sintah yeye alipozungumza na Amani alisema: “Wale wote ni marafiki zangu, hizi bifu nafikiri kuna ajenda nyingine ambazo mimi siwezi kuzielewa kwa sababu hazinihusu.”
Wema, Diamond na Lulu hawakupatikana lakini nao muda si mrefu watakaa kwenye 18 na kueleza kinagaubaga.

chanzo:globalpublishers

2 comments:

  1. Eheee! Watu kiboko yani mtu anaesabiwa hata mass mass alizokula mjini kuwa yeye niwakuja tu.

    ReplyDelete
  2. sasa wolper unaniabisha kama ni kweli hayo wanayoyasema duuu sasa mpenzi diamond wanini jaman haendani kabisa na hadhi yako. acha wafu wazike wafu wenzao

    ReplyDelete