Tuesday 11 October 2011

LULU AHONGWA NYUMBA NA KIGOGO




SKENDO nzito imerushwa kwa staa ambaye ni sura ya mauzo kunako Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akidaiwa kuhongwa nyumba anayoikarabati iliyopo maeneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam, Ijumaa Wikienda limesheni data.

Awali gazeti hili lilipokea habari kutoka kwa chanzo makini kuwa kwa sasa Lulu anajenga kwani siku chache zilizopita alionekana akinunua mabati na alipoulizwa alisema kwa kifupi: “Niko bize na ujenzi wa nyumba yangu.”

Chanzo hicho kilidai kuwa kilipoendelea kumdodosa Lulu kilibaini kwamba yupo ‘bize’ na ukarabati wa nyumba anayodaiwa kuhongwa huku jina la mbunge mmoja mpenda ‘totoz’ na burudani mwenye maskani yake jijini Dar likitajwa (kwa sasa tunalihifadhi, endelea kufuatilia magazeti ya Global Publishers).

“Moja ya masharti aliyopewa ni kuhakikisha hamtaji mtu huyo kwani kinyume na hapo atatibua mambo,” kilisema chanzo hicho.

UCHUNGUZI WA IJUMAA WIKIENDA
Nusanusa ya gazeti hili ilibaini kuwa ni kweli Lulu yupo bize na nyumba lakini hajengi isipokuwa anaikarabati hivyo imekuwa mikononi mwake ikiwa haijakamilika.

Wiki mbili zilizopita aliiambia safu ya gazeti hili ya Bongowood kuwa mashabiki wake watamkosa kwa sababu atasimama kuigiza kwa muda.
Ilibainika kuwa kusimama kuigiza kunasababishwa na ishu hiyo ya ukarabati wa mjengo huo.

MAHOJIANO YA IJUMAA WIKIENDA NA LULU
Kama kawa, kama dawa, ili kupata mzani wa habari hiyo kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Lulu ili kupata undani wa ishu hiyo ambapo mahojiano yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Haloo, nazungumza na Elizabeth Michael ‘Lulu’?
Lulu: Ndiyo, kwani nani mwenzangu?

Ijumaa Wikienda: Mwandishi wa Ijumaa Wikienda.
Lulu: Eeh, leo mna lipi tena?

Ijumaa Wikienda: Kwanza hongera kwa kumiliki mjengo wa maana Mbezi ya Kimara!
Lulu: Duh, na nyie mnajua kunusa mambo ya watu!

Ijumaa Wikienda: Ndiyo kazi yetu, lakini tunasikia hiyo nyumba umehongwa na mheshimiwa mbunge (huku akitajiwa jina).
Lulu: Ni kweli nipo bize na ujenzi wa nyumba yangu ambayo ipo Mbezi ya Kimara. Chondechonde sijahongwa na mtu yeyote, nimejenga kwa pesa zangu ninazopata kutokana na uigizaji.

Ijumaa Wikienda: Habari zilizoenea mtaani zinasema umehongwa na mheshimiwa (huku akitajiwa jina).
Lulu: Najua hao ni wanafiki wasiopenda maendeleo ya watu. Kwani siwezi kutenga pesa za kujenga nyumba hadi nihongwe?

Ijumaa Wikienda: Lakini kwa nini wakuhusishe na huyo mheshimiwa mwenye kitambi?
Lulu: Namfahamu huyo mbunge kama mdau wa sanaa, lakini siyo vinginevyo.

Ijumaa Wikienda: Je, unaweza kutusaidia kupata picha za hiyo nyumba ili tujue ni ya kistaa kiasi gani?
Lulu: Najua mashabiki wangu wanahitaji kuuona mjengo wangu, nawaomba wawe wavumilivu, nikiumaliza nitafanya pati ya ufunguzi na siku hiyo nitawaruhusu kupiga picha.

chanzo:gpl

No comments:

Post a Comment