Monday 3 October 2011

HATIMAYE DIAMOND AMVALISHA PETE YA UCHUMBA WEMA

haya wadau pete ndo ishatulizwa kidoleni

maneno ndo hayooo juu ya cake ya kuzaliwa ya bwana alumasi aliyopewa na mchumba wema

Haya ukisikia nazi imepata mkunaji basi ndio hapo juu,baada ya kusemwa ya kusemwa na mikasa miingi ya hapa na pale sasa bwa mkubwa alumasi kaonyesha kwamba hayo maneno ya binadaamu ni kama kumuimbia wimbo "ZEZE" wa T.I.D mbuzi
bwana alumasi kakata mzizi wa fitina kwa kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wema licha ya yote walimwengu wanachosema.
haya tena blog ya isaackin inampa hongera saana bwa mdogo wetu huyu kwa kufanya maamuzi magumu na kufikia hatua hiyo,
swala la mapenzi ni la wawili na kama yeye alumasi alivyosema kwamba ingawa watu wanaongea ubaya wa wema yeye hauoni na wala hajawahi kufanyiwa ubaya huo,hivyo sometime walimwengu tunamfikiria vibaya tu wema na maybe ni binti mzuri tu na ni wife material kama akipata nafasi ya kupendwa inavyotakiwa.
nani anajua kama wema kote alikotoka na alikopitia ni makosa yake ama ya hao aliowaacha??
hatuwezi ku-judge maybe hao aliowakimbia ndio wenye makosa
hongera sana bwana alumasi kwa kuwa na moyo wa kiume kwa hatua hiyo,lakini ujifunge mkanda vizuri maana sasa ndio kipindi ambacho utakutana na majaribu ya kufamtu toka kwa "mapendenjee" na hela zao za wizi zisizo na kazi.
kama vipi kuweka ulinzi wa kutosha muhamishie mchumba wako mbagaraaaa rangi tatu kabisa maana huko safari ndefu jamaa watasikia uvivu kuja na wataogopa kupigwa nyembe.

BIG UP SANA DIAMOND 

1 comment:

  1. oya we isaack ini mwambie mwenzoo huyo dar to stockhl atuwekee sehemu ya kutowa maoni yetu kama wadau. sasa iyo ni blog au sehemu ya matangazo mwambie achukuwe mfano wako na wengine asiogope matusi pumbavu mbona wewe ushayazowewe mwambie kama kashindwa afunge blog.

    ReplyDelete