Sunday, 30 December 2012

NGOMA YA MWAKA MPYA!

CATHERINE MASUMBIGANA ATWAA TAJI LA UNIQUE MODEL OF THE YEAR 2012



Mwanamitindo namba kumi na mbili kiunoni Catherine Masumbigana ameibuka mshindi wa shindano la Unique model 2012 akifatiwa na Cecilia Emanuel huku nafasi ya tatu ikiend kwa Amina Ayoub.


 Mwanamitindo Mwajabu Juma akimvisha taji mshindi wa Unique model- photogenic Elizabeth Pertty baada ya kutangazwa.
Red carpet yetu ilikuwa hivi.
 Balozi wa shindano la Unique model Roseminner akimvisha taji mshindi Catherine Masumbigana baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2012.

source.uniquentertainment

Saturday, 29 December 2012

BATA KWA VUMBI DEKULA-HOME GROUND


                                                                          Mathias"the don" na mdau

                                                     Lomu"masai"Bizzy body akifurahia yake
                                  majembe Vumbi,Sammy Kasule na Bobo sukari wakiamsha amsha

Boboo na Mdau wakila sebene linaitwa"KUWA INAUMWA,KUWA INAUMA"moja ya seben zinapendwa sana na wakenya na Tz


                                                 "The Don"Mathias toka pale Mlogolo
                                                                                     full nyomii
mtaalam wa kukaanga chipsi

                                                   mi nilikua na mjomba hapa tunafurahi tu
                                                                      Masai kashasahau km kuna  Loliondo

Sammy Kasule "bass guitar"

                                                               Boboo sukeri "singer"
                                 Mtaaalam wa kinanda,na siku hii mzee alikipa haki yake angalia video HAPA CHINI



video haina sound nzuri lakini utaweza kupata utamu uliomo

                                                                              Kasule
                                                              Dekula Vumbi mtamboni

                             HAYA TUONANE PALE WADAU WIKI IJAYO TAR 4-5-JAN 2013

duh!bongo hii

Friday, 28 December 2012

SFI teachers need better education: expert


SFI teachers need better education: expert


The requirements for teaching a Swedish language course for immigrants (SFI) are far too low, according to experts who recommend doubling the teachers’ education.

With Sweden’s recently introduced teaching certificate, studying just one term of Swedish as a second language is sufficient to become an SFI (Svenska för invandrare) teacher.

“If we want SFI teachers to be reasonably competent, the requirements ought to be at least double,” said the government’s SFI investigator Christer Hallerby to Sveriges Radio (SR).

While one term of Swedish as a second language is enough for SFI, teaching a subject in middle school requires studying that subject for three terms.

However, if the requirements are raised it may be difficult to find teachers.

At least 60 percent of SFI teachers must be certified and reach the minimum requirements, and according to representatives from Södertälje’s SFI education, it’s hard enough to find qualified teachers today.

“It would be very hard, at least at first. Unless the job becomes more appealing, so that more people want to become certified,” Jussi Koreila, principal of the SFI education in Södertälje, told SR.

Inga-Lena Rydén heads the National Centre for Swedish as a Second Language at Stockholm University. She also believes finding teachers may be difficult, but even so, remains critical of the low requirements for a job which often requires teaching illiterate students.

“I’d say that this is the most difficult teaching assignment you could have. You have to be able to alphabetize people who come from what we call spoken environments,” she said to SR.

She suggests an alternative to low competence requirements: giving SFI schools more time to find competent teachers.

“SFI teachers could have been exempt from the certification requirement, and been given more time, instead of just lowering the requirements, which I find hard to understand. Lowering the requirements means lowering the value of the subject, which is unfortunate from a societal perspective.”
TT/Clara Guibourg (news@thelocal.se)

DIAMOND AKIKAMUA LIVE DAR CHRISTMASS

MTWARA NAKO WALIPOAMUA KUTOA KERO ZAO KUHUSU GESI


                          picha na mabango vinaongea,hakuna haja ya kuongeza chochote

Thursday, 27 December 2012

TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAAMUZI YA BARAZA LA MADAKTARI KUHUSU MADAKTARI WALIOGOMA





UTANGULIZI
Kutokana na mgomo wa madaktari uliotokea kati ya tarehe 23 na 29 mwezi juni 2012.Wizara iliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la madaktari Tanganyika ili lifanye uchunguzi kuhusu madaktari hao .Idadi ya madaktari wote waliogoma walikuwa 394, kati yao madaktari 376 walikuwa ni madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo (Interns) kutoka hospitali za Muhimbili, K.C.M.C. Bugando, Mbeya Rufaa, St.Francis - Ifakara, Dodoma, Temeke, Mwananyamala, Amana, Haydom na Sekou Toure. Aidha, Madaktari waajiriwa(Registrar) 18 walishiriki katika mgomo huo kutoka hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Baraza lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo.  Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna Madaktari ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
  • Waliofutiwa mashitaka madaktari 49
  • Waliopewa onyo  madaktari 223
  • Waliopewa onyo kali madaktari 66
  • Kusimamishwa kwa muda madaktari 30
  • Mashitaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria madaktari 4
  • Mashitaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza madaktari 22
Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari.   Wizara pia imeridhia kuwapa Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa.  Hata hivyo fursa hii haitawahusu Madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
HITIMISHO
Kwa taarifa hii madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa usajili  na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo. Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ili kupewa barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.  Barua hizi zitatolewa  kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote walio katika mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vya awali  ifikapo tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa kwa kipindi kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote waliopewa adhabu wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu hiyo ilivyotolewa.

Nsachris Mwamwaja
Msemaji
WIZARA YA AFYA NA USTAWI  WA JAMII
27/12/2012

Saturday, 22 December 2012

UMEJIANDAA VIPI NA CHRISTMASS HII!


unapata hii viva chrismas toka kwa baba gaston tukiendelea na storo



svensk julbord,mdau bufee la krishmash hilo sijui kama unaona msosi hapo maana mi kama naona mawenge tu.

                                      mitaa ya malkia leo hii mchana


i can see this from my balcony

 
 mmh!nimemfikiria huyu mnyama ila bei yake ni mahari kabisa huko home unachukua mke kigori tena kwa mbweeembwe ukijitambulisha isaackin.kibopa.com

hapa ndio huwa naanzia mara tu nnapodaka jasho langu.thanx god kwa kunipa hili wazo
 

 ofcourse snow ikianguka vyombo navyo vinaadhibiwa inabidi vikae nje kwenye snow vipigwe baridi kama sisi vibosile wao,vikitoka hapo vinakua nachurale kama udasi unaujua?km huujui muulize Mjengwa.

kwa sisi wengine tulio na familia hilo si jambo la kuuliza maana huu mwezi huwa ni wa kununa kwa sababu namba za kamshahara haka tunakatafuta kwa mbinde huwa zinafutika kimiujiza,maana hata uwe na mamilioni utashangaa ngoma ina read 4000000,mara 400000,mara 4000,mara 400,mara 40 na ngoma ikifika hapo mara nyingi kunakua na arlet kichwani kwamba sasa ndio unakanyaga maars! maana baada ya hapo itasoma 00.00/= cash.

unabaki na risiti rundo ukihesabu mara ishirini ishirini bila kuamini kama ndo zimekwenda hivyo,lakini bahati mbaya hii inakua zimeenda kweli hamna ndoto zile kama za Obama eti"i have a dream".det är ingen dröm kompis

haya ukijifikiria vizuri kunakua na wiki kama 5 hivi za kununa na kuwa serious mpaka uje kucheka tena.bahata mbaya sana huku hamna mazabe kama utafanya upate ziada no,tunaenda date kwa date no digit.
kwa sisi wengine wenye familia huku na kule ndio inakua dangee zaidi maana zile sarakasi tulikua tunarukia mabinti wa watu result ndo sasa inabidi kote utoe huduma zinazofanana.
kwa hapa ugenini tunajaribu jaribu kuiga utamaduni tena japo kwa kulazimisha si unajua tena badae na sisi tunaweza kuitwa kina Isaac Mwaikololosson.

Basi na utamaduni huu mpya sikukuu kama hii mila na utamaduni inabidi siku hiyo kila mtu anaenda na paåsee imejaa zawadi ukialikwa kwenye christmess dinner.
maana lazima umnunulie kila mtu kitu,and yes naww wanakuletea zawadi.sasa na hivi vi-kurona vyetu vya mawazo hii inakua ni kama kitanzi vile
anyway hamna jinsi unajikusuru na sio mbaya kwa mwaka mara moja and im happy for it,hata kama inasoma noll punkt noll noll.

kwa wale wenzetu mlio nyumbani tunawaombea heri ya afya tena maana maralia nayo haichezi mbali.
ofcourse siku hiyo tunajua ni kama utamaduni wa siku zote tumezoea huko,kwanza kushiba pilau sana,watoto wakashushia na soda,na wakubwa sijui maana nnavyoelewa pilau ukashushia na safari bier utasababisha tsunami.baada ya hapo utamaduni ni kwenda punga upepo mwanaaana wa bahari ya hindi ingawa sometime kunakuwa na harufu za pronto hapa na pale lakini aah siku inaenda na amani moyoni.
ndio hivyo bandugu binadamu kila siku haturidhiki hivyo tunachopata tumshukuru muumba kwamba japo tuko hai hivi vingine ziada tu.haya mi ndio naelekea kujipa u-bizzy-boddy mpaka next week ndio tutaonana maana hapa labda kutakua na salamu za hapa na pale kushtuana.

bila kusahau Awilo Longomba yuko hapa kutuchezesha seben la kufungia mwaka.kwa habari hiyo zidi soma poster hapo juu.

REMEMBER DNT DRINK AND DRIVE UTAKUFA

MTANZANIA JOYCELINE MARO AIBUKA MSHINDI MISS EAST AFRICA

 Mrembo wa Afrika Mashariki 2012  (Tanzania),Jocelyne Maro (katikati) akiwa na mshindi wa pili (Uganda),Ayisha Nagudi pamoja na Mshindi wa tatu (Burundi),Ariella Kwizera mara baada ya kupatikana kwa washindi hao katika Shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mrembo wa Afrika Mashariki 2012  (Tanzania),Jocelyne Maro akiwa na washindi wenzake alioingia nao hatua ya tano bora katika Shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Warembo walioingia hatua ya kumi bora.
 Mrembo wa Afrika Mashariki 2012  (Tanzania),Jocelyne Maro akipungia mkono mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Pongezi kutoka kwa Washiriki wenzake.
 hamaki ya ushindi ........
Warembo wakipita na vazi la Ufukweli...
 Muandaaji wa Shingano la Miss East Africa nchini Tanzania,Rena Calist akitangaza majina ya washindi wawili walioingia hatua ya tatu bora.

Majaji wakijadiliana jambo wakati wa hatua ya kumi bora.
 Burudani kutoka kwa Mzungu Kichaa. 
 Burudani kutoka kwa Mad Ice. 
MC Geitano akitoa maelekezo wa washiriki walioingia hatua ya tano bora.
 Wadau mbali mbali walifikika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kushuhudia Mrembo wa Afrika Mashariki anavyopatikana.
 
SOURCE:MATUKIOMICHUZI