Tuesday, 28 May 2013

ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA GHAFLA

Mangwair akiwa katika pozi na msanii M2 the P
Taarifa zilizotufikia ni kwamba msanii Albert Mangwair asubuhi ya leo alipelekwa hospitali pamoja na msanii M2 the P ambaye kwa sasa yupo hoi katika hospitali ya St Hellen Afrika Kusini. Mangwair amepoteza maisha leo saa 9 alasiri baada ya kupelekwa hospitalini hapo akiwa hajitambui. Kwa mujibu wa Hussein Original aliyeko jijini Pretoria nchini Afrika Kusini ni kwamba Mangwair alikuwa anakaa gheto moja na msanii M2 the P na asubuhi ya leo walienda kuwagongea na kuwakuta wote wamezima katika chumba chao. Mangwair na M2 the P walitakiwa kurudi jijini Dar es Salaam leo. Mungu ailaze roho ya Mangwair mahali pema peponi.
SOURCE:GPL

No comments:

Post a Comment