Thursday 17 March 2011

HELKOPTA KWA BABU LOLIONDO!


waweza kudhani ni maigizo!hapana hakuna maigizo ni kweli watu wamechoka na hali ya maisha na maradhi,
rais hajui matatizo ya wananchi wala ni kwanini wana matatizo.
sasa inapotokea hali yoyote ile ikaonekana kuna ukombozi watu wanakimbilia huko,ukienda hospitali  madawa  hakuna unaambiwa ukanunue dukani ukienda huko mchina kajaa tele na madawa yake famba katengeneza kwa unga wa ngano.
umeme mgao,maji hayatoki na bili unalipa.bei za vyakula zinapanda ovyo ovyo.prezidaa yuko jamaica anabembea.makamu wa rais yuko mbugani serengeti na wakeze.waziri mkuu nae sijui anamwakilisha rais kwenye kikao cha wafanyabiashara nchi gani huko.
wabunge bungeni wanapiga usingizi wa pono,wakishtuka wanagonga meza wanataka mashangingi mapya na bajaj kwa wajawazito.spika anapitisha muswada na kesho yake anaitisha kikao na kusema hamwombi mwandishi yoyote msamaha na kwanza anabadili na jina liitwe kizungu zaidi.
mawaziri ndio hao wanatuletea DOWANZI NA RICHMONDO,IPTL,EPA.mizaha mizaha na dharau na ufisadi wa viongozi kila kona tukijashtuka prezidaa kamaliza muda wake CCC wanaiba kura anampasia kijiti mwingine sinema inaendelea.
wananchi wanakufa kwa maradhi,njaa na ujinga bila kusahau mabomu yanalipuka na kuua watu kwa uzembe makambini wanajeshi wamelala kwa ulevi au kushiba kwa mikopo na marupurupu wanayopewa na kusahau majukumu yao.
itafika muda taifa zima litahamia loliondo na kuna mahali watu wataona shida kujiita watanzania .embu ngoja niishie hapo maana.

No comments:

Post a Comment