Thursday 24 March 2011

UCHUKUZI WA MAITI ZA WANAMUZIKI WA 5 STAR



marehemu dr remmy alitoa ujumbe mzuri sana hapa

mnawaonaje hapa,warembo wasafi na wamependeza
baada ya kufariki wanaishia kubebwa hivi kama magunia ya viazi toka uporoto

kwa kweli hakuna kitu kilichoniuma katika msiba huu mzito uliotokea kama uchukuzi wa maiti za wanamuziki hawa.sijui nani alaumiwe hapa.
nimezoea kuona majambazi wakipakiwa kwenye maroli dizaini hii kama wakiuliwa katika mashambulio na mapolisi,nikawa naona ah sawa tu maana wale ni majambazi na ni wauaji.
sasa hii tena kuona wanamuziki hawa baada ya kupata ajali hii nao wakapakizwa katika maroli haya ikanistua sana,imekuwaje watanzania sasa miili yetu imekua haina value kiasi hiki??
kumbe mtu ukifa unakua huna thamani mpaka kufikia kubebwa na magari ya dizaini hii,ni afadhali basi hata ingekuwa ni majeruhi wamepakizwa humo kuwahishwa hospitali ingeeleweka,lakini hawa walishakufa,zilishakuwa maiti,je ilishindikana kabisa arrangement ya usafiri unaoeleweka japo kidogo kwa ajili ya kusafirisha miili hii kwa heshima??
sidhani kama halmashauri yoote ya mkoa wa morogoro walishindwa kupata usafiri jamani nashindwa kuamini.
hili jambo sio la kulikalia kimya sababu halijakutokea wewe.mwenzio akinyolewa nawewe tia maji.hii inaweza kutokea hata wewe unapokumbwa na tatizo kama hili.
ni wakati wa serikali kutambua mahitaji ya wananchi na jinsi ya kukidhi mahitaji hayo.kama kungekuwa na huduma nzuri za hospitali  na ambulance za kueleweka (sio zile bajaji walizonunua maana zitasababisha ajali na kuwaua maiti tena mara ya pili) zingetumika kusafirisha miili hii.
kama angekuwa mtoto wa fisadi mmoja kapata ajali hapo ingetumwa hata helkopta kwenda kumchukua kumwahisha hospitali,hiyo ndio afrika yetu.
tumeona hapo kenya kipindi fulani mtoto wa kibaki alianguka akateguka mguu ni helkopter ya jeshi tena ilitumwa ikamchukue kumpeleka hospitali.
lakini kwa raia wa kawaida wanyonge wataishia kusafirishwa kama hivi mnavyoona hapo juu.nani anajali
laiti kama hawa marehemu wangejua hili nadhani wangejiandalia usafiri kabisa kama remy anavyoimba.

THAMANI YA MIILI YA WATZ SASA INAFANANISHWA NA MAGUNIA YA VIAZI 

No comments:

Post a Comment