Thursday 3 March 2011

HONGERA LADY JAY DEE NA GADNA


nyumbani lounge utakutana na mambo matamu kama haya
ulabu wa kila aina unapatikana kwa akina sisi tunaopenda vimiminika

sehemu za kukaa kibao ni wewe tu na roho yako



 kwa wale mnaomkumbuka mwanadada huyu machachari,mtakumbuka kipindi kileee alipoanza kujitokeza kwenye tasnia ya muziki katika miondoko ya HIP-HOP & RAGA.
ni mwanamuziki pekee wa kike aliyeweza kuimba live miziki ya kina MC LYTE na QUEEN PATRA kama vile ni wanamuziki hao wawili wako pale live,enzi hizo hatukuweza kudhani wala kufikiria kama huyo LADY J.D tumuonaye angeweza kufika hapa alipo sasa.
ni jitihada zake mwenyewe ambazo zimemfikisha hapo alipo ikiwa ni pamoja na kumiliki bendi,maji yenye chapa jina lake,nyumba kadhaa na biashara nyinginezo sasa anakujia na restaurant asilia NYUMBANI LOUNGE.

kujituma,mapenzi kwa fans wake kujishughulisha kwa kubuni miradi na biashara mbali mbali n.k vimeweza kumfikisha hapo alipo sasa.
jamani wanawake mkiamua mnaweza,kinadada wengine wanadhani kubadili wanaume kila siku ndio kujiwezesha,mara leo yusuph,kesho yakobo keshokutwa uko na mwamedi jumamosi una shabani mtondogoo umemkamata luyumba mara umemaliza mtaa unahamia mtaa wa pili ukimaliza na watatu,ukiona vipi unahamishia mlogolo sio ishu wajameni.igeni mfano wa mwanadada huyu.

No comments:

Post a Comment