Wednesday 18 January 2012

CHALZ BABA ASOGEA KWA WEMA

 


MWANAMUZIKI gumzo kwa sasa aliyechomoka katika Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ na kusaini mkataba kwenye Bendi ya Mashujaa kwa ada ya Sh. milioni 15, Charles Gabriel ‘Charlz Baba’, amesogea mtaa anaoishi Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Charlz Baba ametumia jeuri ya mamilioni hayo ya Mashujaa, kusaka nyumba kwa gharama yoyote jirani na anapoishi Wema aliyewahi kuwa mpenzi wake maeneo ya Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Habari za uhakika zilisema kuwa, Charlz Baba amehamia mtaani hapo mita chache kutoka nyumba anayoishi Wema mara baada ya kurejea kutoka Dubai alipokwenda kwa mapumziko mafupi.
Ilidaiwa kuwa dau hilo alilolamba limempa jeuri ya kuyaacha maskani yake ya zamani maeneo ya Block 41 Kinondoni, Dar alipokuwa amepangisha kwa muda mrefu.
Ilibumburuka kuwa, Charlz Baba aliyetambulishwa rasmi kwenye Bendi ya Mashujaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Business Park Kijitonyama, Dar, amechukua nyumba nzima yenye vyumba kadhaa vya kulala, sebule, jiko na bafu ikidaiwa kuwa amelenga kumnasa Wema kimapenzi.
RISASI MZIGONI
Baada ya kumwagiwa ‘upupu’ huo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Charlz Baba ili kupata undani wa taarifa hizo ambapo alikiri kuhamia mtaani hapo.
Alipoulizwa kama ni kweli alihamia eneo hilo ili kumrudisha Wema kwenye himaya yake kimapenzi alisema:
“Mwanzoni sikujua kama Wema alikuwa anaishi mtaa ule, ila nilipoambiwa na madalali kwamba yuko maeneo hayo, nilihakikisha napata nyumba.
“Nilitamani sana kuwa jirani yake. Huwa nafarijika sana kuwa karibu naye, naamini siku moja moja tutakuwa tunatembeleana.”

WEMA KIZIMBANI
Wema alipoulizwa na paparazi wetu kama ana habari kuwa anaishi mtaa mmoja na Charlz Baba, alishtuka na kusema:
“Acha bwana…anakaa nyumba gani? Hebu nielekeze. Ni kweli anaishi mtaa huu?”
Alipoelekezwa hadi mlango wa nyumba anayoishi Charlz Baba mtaani hapo, Wema aliangua kicheko: “Teh…teh...teh.”
Alipoambiwa kuwa jamaa huyo amehamia mtaani hapo ili kurejesha penzi lao kama zamani, Wema aliahidi kumpigia simu mwandishi wetu baadaye ili kulizungumzia hilo.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Wema hakupiga simu na hata alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa.
Wema na Charlz Baba waliwahi kuwa na mapenzi ya njiwa kabla ya Bwa’mdogo wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ kuchukua mtoto.

CHANZO:RISASI

3 comments:

  1. WEWE BWANA UNACHUKUA HABARI ZA UDAKU GAZETI LA UWAZI UNATUWEKEA KWENYE BLOG YAKO ,SIKUIZ HUNA MPYA NINI.HIZO TUSHAZISOMA GAZETINI HUMO.TULETEE MAMBO YAMAANA KAMA HIYO YA MIKOBA YA KISWEDE NIMEKUPA POINT HAYA MAMBO YA UWAZI UYAACHE UWAZI,MDAU SWEDEN,

    ReplyDelete
  2. KITU CHA KWANZA NAKUSHAURI MDAU HAPO JUU NI ACHA JAZBA,CHA PILI NI KWAMBA KM WEWE UMESOMA HII HABARI HUKO GPL NI SAWA LAKINI HAPA TUMEWEKA SABABU KUNA WADAU AMBAO HAWAIJASOMA KULE.VILE KWAMBA SINA MPYA INAWEZKANA MAANA NILISEMA HAPO NYUMA KM WE NI MFUATILIAJI WA BLOG KWAMBA IMEBIDI BLOG IENDANE NA MAZINGIRA YA KIBONGO SABABU INTERNET NI LONGO LONGO KM UMEME NA MAFUTA.BY THE WAY HATA HABARI YA PASS ZA KISWEDE IMEKOPIWA KWENYE GAZETI LA UDAKU LA KISWEDE .SASA UNGESEMA UMESHASOMA NA HIYO INGEKUWAJE?KINGINE NAKUSHAURI UNAPOKUWA NA HABARI YOYOTE TUTUMIE HAPA NASI TUTAIWEKA,
    HALAFU "KIVUE KIATU"

    ReplyDelete
  3. what the meaning of that kivue kiatu misemo yakina khadija kopa hiyo.haikufai hiyoo , ISSAKING. nimekupa chalenge tuu sina bifu nawewe na wala sikutaka maneno hayo sijui kivue kiatu hata sielewi manake,mana sipengadi mambo yakiswahili kihivyo kupashana kusutana sijui,anyway forgiving me kama nimekukwaza kukuambia usituwekee mamboya GLOBAL PUBLISHERS.nilijua natoa ushauri kumbe nimekukwaza,so sorry bro.ila ujue mimi pia nimmoja wa Fans wa Blog yako .kumbe hupendagi ushauri samahani bwana mzee.salimia familia yako .byee

    ReplyDelete