Friday 6 January 2012

MAJAMBAZI YASHAMBULIA NDEGE ILIYOBEBA DHAHABU KWA JARIBIO LA KUPORA,MMOJA AUWAWA




Pichani: Wakazi wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wakiangalia mwili wa mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi (jina hajafahamika), akiwa ni mmoja wa watu wanne waliyovamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), akiwa amekufa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika jaribio hilo la kutka kupora dhahabu jana.


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha nzito za kivita, wamevamia Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), na kuiteka ndege ndogo iliyokuwa imebeba dhahabu kutoka mgodini hapo, kwa ajili ya kuikisafirisha kwenda nje ya nchi.
Tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa 5:55 asubuhi, katika uwanja wa ndege wa mgodi huo uliopo umbali wa kilomita 5 kutoka katikati ya mji wa Geita, na kwamba majambazi hayo yaliyodaiwa kujifunika nyuso zao, yaliishambulia ndege hiyo kwa risasi za moto, kwa lengo la kutaka kupora dhahabu hizo zenye mabilioni ya fedha.
Habari kutoka eneo la tukio zilizoifikia FikraPevu, zinaeleza kwamba, wakati majambazi hayo yakiimiminia ndege hiyo risasi, huku yakifyatua ovyo risasi nyingine hewani, askari polisi Wilaya ya Geita walifanikiwa kufika eneo hilo haraka, kisha kuanza kupambana na watu hao kwa risasi za moto, kabla majambazi hayo hayajakimbia na kuliua jambazi moja.
Katika majibizano hayo ya risasi, askari polisi walifanikiwa kuliua jambazi moja baada ya kulimiminia risasi kifuani, na kwamba kabla ya jambazi hilo kuuawa na polisi lilikuwa limejeruhiwa vibaya na mmoja wa walinzi wa mgodi huo ambaye ni raia wa nchini Afrika Kusinia.
Dhahabu iliyonusurika kuporwa na majambazi hao inadaiwa kuwa ilikuwa ni zaidi ya kilo 1,000, ambapo ilikuwa imegawanywa katika maboksi 16 huku kila boksi moja likiwa na matofali manne ya dhahabu, na kwamba kila tofari moja linadaiwa lilikuwa na ujazo wa kilo 25.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio na kuthibitishwa na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la polisi wilayani humo, zimeeleza kwamba, uchunguzi wa awali umeonesha kuwa majambazi hayo yapatao wanne walivamia mgodi huo kwa kuingilia geti kuu la kuingilia kwenye uwanja huo wa ndege wa mgodi wa GGM kabla ya kuiteka ndege hiyo.

“Ilikuwa kama sinema vile, maana majamaa (majambazi), yalikuwa yanarusha risasi nyingi kwa kuishambulia ndege hiyo iliyokuwa ikipakia dhahabu. Baadaye polisi walipofika walipambana nayo kwa risasi za ana kwa ana na jambazi moja tumeliua”, alisema afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la polisi wilaya ya Geita kwa njia ya simu.
Imeelezwa kuwa majambazi hayo yakiwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, bunduki aina ya SMG, pamoja na Bastola, walianza kuishambulia ndege hiyo yenye nambazi za usajili SH-TZX iliyokuwa ikipakia dhahabu kutoka kwenye gari maalum iliyokuwa imebeba dhahabu hiyo kwa kuirushia risasi nyingi mfululizo.
“Inadaiwa kwamba, baadhi ya walinzi wa mgodi huo waliokuwa katika eneo la tukio wakihakikisha usalama wa mali iliyokuwa ikisafirishwa, wengi wao walilazimika kutimua mbio baada ya majambazi hayo kuanza kutoa mashambulizi ya risasi, na kwamba katika walinzi hao alibaki mzungu mmoja raia wa Afrika Kusini ambaye ni mfanyakazi wa mgodi huo aliyekuwa na bastola ambaye alianza kupambana na majambazi hayo kwa kuyarushia risasi.
Inadaiwa kuwa wakati mzungu huyo akijibizana kwa risasi na majambazi hayo, mmoja wa majambazi hayo alijikuta akiishiwa risasi na kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi kwenye mkono wa kulia na kulazimika kukimbia kuokoa maisha yake, na baada ya muda mfupi askari polisi walifika na kuanza kupambana na majambazi hayo.
Hata hivyo imebainishwa kuwa baada ya askari kufika majambazi watatu yaliamua kukimbilia kwenye msitu mkubwa unaozunguka mgodi huo, ambapo jambazi moja lililokuwa limejeruhiwa na Mzungu huyo kushindwa kuhimili vishindo vya askari polisi kabla ya kuuawa.
“Wakati polisi wanafika eneo la tukio, majambazi matatu yalitimua mbio msituni. Lakini mmoja aliyekuwa amejeruhiwa alibaki akirushiana risasi na polisi, na baadaye alitwangwa risasi akafa papo hapo. Hili ni tukio la kwanza katika mgodi huu”, alisema ofisa mwingine wa jeshi la polisi kwa sharti la kutotajwa jina kwa vile siyo msemaji.
Jambazi aliyeuawa bado hajatambuliwa jina, na alikutwa na basotola moja aina ya Chenese yenye namba za usajili 0048467, ikiwa na risasi sita, bunduki moja aina ya SMG yenye namba za usajili za Uganda UA.89381997, Mabomu manne ya kutupa kwa mkono, Magazini 4 pamoja na risasi 60 ambazo hazijatumika, huku akiwa amevalia nguo za kawaida seti nne ndani na ile ya tano (juu), ikiwa ni sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Hata hivyo imeelezwa kwamba, mfanyakazi mmoja wa mgodi huo ambaye ni raia wa Afrika ya Kusini aliyetambuliwa kwa jina la Engenas Van Der Schuffs, alijeruhiwa kwa risasi na majambazi hayo, baada ya kumpiga risasi kwenye mkono wake wa kulia na kumjeruhi vibaya.
Marubani wa Ndege iliyoshambuliwa yenye nambazi za usajili SH-TZX wametambuliwa kwa majina ya Meja Kondo Hamza pamoja na Hamdan Salehe, na kwa taarifa zilizopatikana kutoka Geita zinaeleza kwamba ndege hiyo imeshindwa kuondoka kwenye uwanja huo kutokana na moja ya mabawa yake kutobolewa kwa risasi na majambazi hayo.
Hilo ni tukio la kwanza mkoani Mwanza kwa majambazi kuteka mgodi na kuishambulia ndege kwa risasi, ikiachiliwa matukio mengine ya uhalifu ambayo yameonekana kuanza kurudi kwa kasi mkoani hapa.

chanzo:fikrapevu

HAYA HATIMAYE SASA TUMEJUA KUMBE VIPANDE VYA DHAHABU TANI MOJA HUWA VINASAFIRISHWA KWENDA SOUTH AFRICA KILA WIKI??NA HUKU VIONGOZI WETU WAKIKAZANA KUTEMBEZA BAKULI KILA KUKICHA KUOMBAOMBA VITU AMBAVYO KWA DHAHABU HII INAYOTOKA HAPA TUNGEUZA WENYEWE  TULIKUA NA UWEZO WA KUVINUNUA.
HAPO NDIO HUWA NAJICHUKIA KUWA MUAFRIKA

SASA HAPO MWIZI NANI?HAO WALIOUWAWA AMA WALE WASOUTH WALIOONDOKA NA DHAHABU?


1 comment:

  1. Wasouth waliondoka na dhhbu tehe tehe.Ama kweli wajinga ndiyo waliwao!!!!!!

    ReplyDelete