Friday 6 January 2012

KUNA UKWELI HAPA

            Eti Bongofleva, ...kwani lazima mdundo huo?    
 Friday, 06 January 2012 21:38
0digg
Katika mambo ambayo sijaweza na nahisi sitakuja kuweza ni zile stepu za kwaito ambazo kila nikiingia disko siku hizi nakuta watu wananidensia, nimetokea kuzichukia sijui kwa sababu gani, zikianza zile tu ndio kiwango cha kilevi kinaongezeka.Sisemi kwamba ni aina mbaya ya muziki, msinielewe vibaya ila ninachokigundua hapa ni kwamba wamezidi...
Khe!
Kwaitoooo, kwaito, kwaito yenu?
Mnaijua ilikotoea?
Kwa nini msitwange mnanda hapo tukajivunia utanzania wetu jamani tunakuwa watu wa kutukuza vya kuja? Kumbe mnajua kubuni staili na kuzidensi freshi namna hile kwa nini staili hizo msiziweke kwenye mnanda na sisi wakatutambua?
Nahisi kuna fikra za kitumwa katika hili ingawa mlengop najua ni wa kibiashara zaidi.
Sasa ukija na hawa wanamuziki wa hiki kizazi ndio kabisaaa, kila itakayodondoka, ndio hiyo hiyo midundo nimeshangaa mpaka juzi mpaka ngoma mpya ya Profesa Jay inagongwa katikati ya Kwaito na wanaicheza kwa staili ile ile.
Dah...
Huyu si heavyweight Mc jamani mbona mnamfanyia hivyo?
Naomba niwape ushauri mkubwa mzuri nikiwa kama rafiki wa karibu wa hii aina ya muziki ambao kila mtu anaifurahia, nasema hivi, ..tujaribu kuangalia na muziki wa nyumbani nao kama tunaweza kuushikia bango namna hii.
Au sio jamani?
Chukueni Mnanda nao muutwange kama hivi halafu muone kama watu wataucheza ama watauacha. Hivi mnajua kwamba watu wanawasikiliza nyie kiukweli?
Haya nawatakia kila la heri na shughuli zenu zan ujenzi wa taifa.

No comments:

Post a Comment