Thursday 12 January 2012

WEMA APANGISSHIWA NYUMBA NA BILIONEA!



 NYUMBA HIYO INAYODAIWA KUPANGWA NA BILIONEA


Kila kitu cha Wema Sepetu kimebadilika, mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea mkubwa Dar (jina tunalo) kudaiwa kujitosa kumlea mrembo huyo akianzia kwa kumpangishia nyumba ya kifahari.
Habari kutoka kwa vyanzo vyetu zinadai kuwa bilionea huyo amempangishia Wema nyumba hiyo eneo la Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam.
“Wema ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa na kukubali kufujwa mpaka azeeke,” alisema mtoa habari wetu ambaye ni ‘shostito’ wa Wema na kuongeza:
“Mtu na hela zake ameingia kwa presha kubwa, ameahidi kumpa matunzo ya nguvu. Mbali na kumpangia nyumba, ameahidi pia kumnunulia gari la kutembelea.”
Chanzo chetu kingine kilipasha kuwa Wema kwa sasa amekata shauri la kuacha kujihusisha na mapenzi ya vijana wadogo kwa sababu wengi wao wanakuwa hawajaamua kutulia kufanya maisha.
“Hata sisi wenyewe kama marafiki zake tumemuunga mkono na tumemshauri azingatie hilo. Unajua inauma sana kupoteza muda kuwekeza upendo wako kwa mtu ambaye hana mapenzi au mtu ambaye bado anawaza kurukaruka.
“Hayo ndiyo ambayo Wema ameyatafakari na anajutia muda wake ambao aliupoteza kwenye mapenzi yasiyo na uelekeo,” kilisema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Wema ameamua kuanza upya kwa kila kitu ili kutibu majeraha ya moyo aliyoyapata baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Utata kuhusu mahali ambapo Wema amepata fedha za kupanga nyumba, upo hata kwa mama yake mzazi, Mariam Sepetu ambaye aliliambia Amani kuwa ameshindwa kumbana kwa sababu ni binti mkubwa hivi sasa.
“Wema aliposema anapanga, mimi na mjomba wake tulimuweka chini atuambie uwezo wake wa kupanga nyumba, fedha amepata wapi na amejipanga vipi kuendesha maisha ya kujitegemea.
“Alitujibu kwamba anapanga nyumba mwenyewe. Tulimkatalia na kumtaka aishi nyumbani lakini alikataa kwa maelezo kuwa hawezi kuishi nyumbani miaka yote kwa sababu amekua. Tumemkubalia na mimi mama yake nimeshindwa kumbana zaidi kwa sababu amekua,” alisema Mariam.
Jitihada za mapaparazi wetu kumpata Wema atie neno kuhusu ‘mchanyato’ huo, ziligonga mwamba, kwani simu yake ilikuwa haipatikani na hata alipofuatwa nyumbani kwake mara nne kwa siku mbili mfululizo hakuwepo.
Wema, ameanza maisha mapya ya kujitegemea baada ya kuwekana kando na aliyekuwa mchumba wake, Diamond.

CNAZO:GLOBALPUBLISHERS

No comments:

Post a Comment