Tuesday 31 January 2012

KIZUNGUMKUTI CHA HABARI

                              Kwanza imetoka habari hii leo   (JK ABARIKI POSHO ZA WABUNGE)

                                                                             halafu ikaja hii 

                                  TAARIFA MAALUM KUTOKA IKULU:

              Rais Jakaya Kikwete Hajabariki Swala La Posho Za Wabunge



      

Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao: 

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.

Mwisho.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012 
***********************
 
 
 toka isaackin
OKAY MWANANCHI WA KAWAIDA BADO NAENDELEA KUSUBIRI HAPA NAJUA ATAKUJA KIGOGO MWINGINE NA TAMKO JINGINE LA KUTUSHANGAZA ZAIDI  KAMA SIO KUTUCHANGANYA


No comments:

Post a Comment