Monday 9 January 2012

ndikumana kuandaliwa fumanizi



Baada ya Uwoya kufunguka namna mwanamke huyo (shoga’ake) alivyomuibia ‘mali’ zake katika gazeti pacha la hili, Ijumaa toleo namba 755 la Januari 6 hadi 12, 2011, inadaiwa kuwa Janeth alipata wakati mgumu kutokana na mume wake kuhitaji majibu ya kueleweka na kusababisha ndoa yake kuwaka moto.
Katika habari hiyo, Uwoya alitamka laivu kuwa aliwafuma Janeth na Ndikumana katika mazingira ambayo huhitaji kuambiwa kwani kama hujui kusoma, hata picha huwezi kuangalia?

MAANDALIZI YA FUMANIZI
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya Janeth, kuna kila dalili endapo Ndikumana ataendelea ‘kumsumbua’ mwanamke huyo kama alivyodai, ipo mikakati kabambe ya kutokea fumanizi la kihistoria.
“Ninavyomjua mume wa Janeth ana wivu sana kwa mkewe, lazima atamwekea Ndikumana mtego wa fumanizi ili amuaibishe,” kilisema chanzo chetu.

IJUMAA WIKIENDA KULETEWA PICHA ZA FUMANIZI
“Ni kiasi cha kumwambia Janeth amkubalie tu ‘then’ wakiingia chumbani, wanavamiwa na kupigwa picha, msijali zitaletwa kwenu (Ijumaa Wikienda), mtaziona na mtakuwa wa kwanza kuripoti.”

KWANI JANETH AMEOLEWA?
Kuhusu kuwa na ndoa yake, tena mbichi, Janeth alifunguka: “Jamani nina ndoa yangu, nimeolewa mwaka jana kule Madagascar ninakoishi na mume wangu ambaye ni raia wa Kongo-DRC. Kwa sasa nipo Dar kwa mapumziko, lakini baba watoto ni mfanyabiashara ‘so’ yupo Burundi na Rwanda kikazi.”

HALI ILIKUWAJE BAADA YA UWOYA KUCHAFUA HALI YA HEWA?
“Mume wangu alipata habari na wengine walimpelekea gazeti ‘so’ amekasirika sana, kaniambia anakuja Dar sijui hata itakuwaje.
“Nilipokea simu nyingi sana, kuna mtu aliniambia Irene (Uwoya) ananitafuta, yaani Bongo imenishinda, ngoja nirudi zangu Madagascar kabla hayajanikuta makubwa kwani namjua mume wangu alivyo mkali.”

BADO HALI SI SHWARI
Hivi karibuni Uwoya na Ndikumana waliingia kwenye gogoro zito huku ndoa yao ikidaiwa kutibuka ambapo hadi sasa hali bado si shwari.


chanzo;gpl

No comments:

Post a Comment