Thursday 26 January 2012

VAZI LA TAIFA!

kuna hii kitu hivi sasa imeibuka katika kila vyombo vya habari swala ni kuhusu vazi la taifa,drama huwa haziishi kwenye hii nchi maana kila siku huwa kunaibuka kitu kipyaa.

kuna kipindi iliibuka mara kwababu loliondo,mara  freemason, mara samaki wenye sumu(washauzwa siku nyiingi),mara vitunguu swaumu  vilivyoeksipaya toka china(vishauzwa hivyo)na nishaviona masokoni bongo hii hii.mara posho za wabunge,mara mafuta kupanda na kushuka bei,mara umeme umepanda(hapa nadhani na maji yanakuja kupanda soon)

kushaibuka kila aina ya viroja na statement za ajabu toka kwa viongozi wetu tofauti katika nchi hii,kila siku ni mwendo wa "ametoa kauli,amesema,katoa hotuba,aliwaambia,amezindua,akatanabaisha",mradi purukushani tu za misemo na matamshi lakini kinachofanyika katika mambo muhimu hakuna.

imekua kama vile tuko ndani ya basi bovu ambalo halina dereva.

haya kwasasa kuna hili jipya la kuhusu vazi la taifa,kwasasa imekua ndio nyimbo kutwa kucha.vazi la taifa,vazi la taifa,cha ajabu kumbe kuna watu na kamati ilishapewa hii kazi kutafuta vazi la taifa toka mwaka 2004,unaweza kuamini katika muda wote huo hawajapata uvumbuzi?na sidhani kama hivyo vikao vyao vya kutafuta hilo vazi walikua wanakaa bure,lazima kuna fungu limeliwa hapo na linaendelea kuliwa.

cha kushangaza kuna jingine nalo sijui liliishia wapi,kuna kipindi liliibuka swala la vitambulisho vya taifa hivi liliishia wapi?mpaka sasa hivi hatuoni cha vitambulisho vya taifa wala hata vitumbua vya taifa.

na sijui baada ya hili vazi la taifa itaibuka nini mweeh!

serious imefika muda inabidi viongozi wetu wabadilike na kuwaonea japo aibu wananchi maana tunakoenda sasa sio kuzuri,hizi nyiimbo jamani nyiiimbo za viongozi zimeshawachosha wananchi maana sasa mwanachi wa kawaida ana njaa ya kufa mtu nawewe unamuimbia risala zako kurasa ngapi sijui inawezekana kweli?baada ya hapo wewe unakinga mkono na kulamba posho kisha unaondoka na vx lako V8 ye mwananchi anaondoka mtupu anapiga miayo tu kwa kusikiliza risala ya masaa na njaa risala ambayo mnaandikiana script huko.

kuna mambo mengi ya maana ambayo inahitajika uwajibikaji wa hali ya juu kwenu nyinyi viongozi,jana tu hapa tumeona na kusikia madaktari wameamua mgomo na hakuna aliyewasikiliza,sasa anayeumia nani?

nakumbuka walimu walishawahi kugoma weeeh serikali ikapuuza mpaka wakaghairi (unacheza nini mgomo na njaa wp na wp)

ifike mahali viongozi muanze kuwajibika katika mambo ya maana na kujaribu kusikiliza pale wafanyakazi na watendaji wengine wa mashirika ya umma na binafsi wanapokuwa na malalamiko yao.

sio kila siku mnapuuzia na kuishia kutoa matamko na matamshi na vitisho maana itafika siku hakutakua na msikilizaji wala mtekelezaji wa matamshi yenu,na hapo ndipo nguvu ya umma itakapoonekana.

ni hayo tu mawazo yangu ya leo baada ya kushiba ugali wangu na dagaa wa mwanza. 


No comments:

Post a Comment