Wednesday 8 September 2010

ANATAFUTWA MDADA WA KUSUKA NA KUPAKA HINA-FINLAND

Kutakuwa na sherehe ya MTU NI WATU, sherehe ya Utamaduni wa Tanzania huko Finland.
Anatafutwa Mtanzania anayefahamu kusuka na mwingine kupaka hina ambaye yuko tayari kwenda Finland tarehe 17 September kwa shughuli ya kusuka na kupaka hina kama maonyesho ya utamaduni wa TZ siku ya tarehe 18 September. Angalia message hii hapa chini kwa maelezo zaidi.

Ndugu zanguni, 
Kwenye shughuli za Mtu ni Watu tutakuwa na Fashion Show na maonyesho ya upakaji wa inna na usukaji wa nywele. Ninaomba wale wote ambao wangependa kushiriki ( wake, waume na watoto kutoka kokote kule duniani) au wanaowajua wale ambao wangependa kushiriki wawasiliane nami. Kama kuna mtu ambaye anajua kusuka ( hata kwa wastani tu) naomba naye awasiliane nami maana mpaka sasa hivi tumekwama kwenye hilo. Tunategemea kufanya mazoezi ya hiyo Fashion Show wiki moja kabla ya maonyesho yenyewe.

Naomba taarifa hizi tuzisambaze kwa watanzania na marafiki zetu wote

Kama u tayari tafadhali wasiliana moja kwa moja na Bw Hamprey wa Finland kwa barua pepe. humphkalanje@yahoo.co.uk

Ukipata ujumbe huu mtumie na mwingine.

 
.

No comments:

Post a Comment