Thursday 30 September 2010

FERRE GORA KUTUMBUIZA BONGO IJUMAA

 ferre gola
ferre gola mwanamuziki ambaye ametokea kujipatia sifa na umaarufu toka siku nyiiingi kwa sauti yake kali na nyembamba na inayoweza kumtoa nyoka pangoni,ferre ameanza safari ya usanii katika kundi la wenge B.C.B.G enzi hizo miaka ya 90s akiwa mdogo kabisa katika kundi lote.na baada ya kuchomoka hapo akajiunga na bendi karibia zooote kongwe congo unazozijua wewe,na mara ya mwisho akachomokea kwa koffi olomide na kuunda kundi lake ambalo sasa linatamba katika list ya bendi bora congo.nimeikubali kazi yake hasa baada ya kuona concert aliyofanya hivi karibuni kajitahidi sana kuboresha na yes sasa naweza sema yuko class na bendi inaimba vitu vinaeleweka,and well shikito sasa mtu mzima na pamba anazijua he he hee.

 shikitoo
 Mwimbaji na rapa wa Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akihojiwa na wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere, hata hivyo Kiongozi wao mwanamuziki Ferre Gola anatarajiwa kuwasili kesho saa tano za asubuhi na anatarajia kufanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee siku ya Ijumaa akishirikiana na bendi ya Mashujaa inayoongozwa na Mwanamuziki Jado Field Force

flora bambucha
mnenguaji wa mashujaa band(wale wateja wa kwa macheni sio wageni na flora)
wanamuziki mpiga gitaa la Sollo kutoka kundi la Ferre Gola anayejulikana kama Chally Sollo akihojiwa na vyombo vya habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kuwasili kwa ajili ya onyesho lao linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee keshokutwa Ijumaa.

No comments:

Post a Comment